SOMO:
TAMBUA NYAKATI NA MAJIRA
- UTANGULIZI.TAMBUA NYAKATI NA MAJIRA
Utangulizi
Hatima ya mwanadamu imefungwa katika
nyakati na Majira usipotambuwa wakati na majira ya Mungu juu ya Maisha yako
hilo ni tatizo
Tunapozungumza kwa habari ya nyakati na
majira tuna maana hii;
- Majira: Ni vipindi mbalimbali ndani ya wakati ulioamriwa; mfano masika, kipupwe, kiangazi, n.k
- Nyakati: Ni vipindi kulingana na matukio ya makusudi; mfano asubuhi, jioni, nyakati za mwisho, nyakati za utandawazi, wakati wa kupanda, kuvuna, n.k
Ni muhimu sana kufanya kila jambo kwa
wakati na majira yake, mfano kupanda wakati wa kupanda, kuvuna wakati wa
kuvuna, n.k
Siku zote ukifanya jambo nje ya wakati
wake utaonekana kituko, na matokeo yake ni kutokufanikiwa. Kila jambo huonekana
la busara mbele ya wenye hekima likifanyika ndani ya wakati wake, kwa lugha
nyingine, "Everything is right at right time". Maana yake ni kwamba
ukifanya jambo nje ya wakati hata kama jambo hilo ni jema, litabadilika kuwa
baya. Wakati una 'impact' kubwa sana katika jambo lolote. Tazama formula
ifuatayo;
- Luka 19:42 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.
- Kila jambo kuna majira yake na wakati wa kila kusudi,
“Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati wa
kila kusudi chini ya mbingu” (Muhubiri 3:1)
9,000,000 +Nyakati isiyo sahihi = 0
- Kitu sahihi +Muda usiyo sahihi = sifuri
Kitu sahihi +wakati sahihi= na Mazidisho
yaani mafanikio
Kwa hiyo unaweza kuona ni jinsi gani
wakati unavyoweza kuathiri mamboyako hii
ndiyo Kwa hiyo jambo ni jema sana likifanywa ndani ya muda wake. Kwa mfano,
tendo lile lile linalofanywa na wanandoa likifanywa na watu ambao si wanandoa
linakuwa si sahihi.
- Wala tendo halijabadilika, ni lile lile lakini kwa nini likifanywa na wanandoa ni sahihi na likifanywa na watu ambao si wanandoa sio sahihi? Tena limepewa na jina jingine kabisa, uzinzi; na ukifanya jehanamu unakwenda kwa miguu yote miwili. Tatizo hapa ni wakati!
Mhubiri 3:1-3
Hapa mwandishi anajaribu kutueleza kuwa
kila jambo lina wakati na majira yake, tena kila kusudi. Anasisitiza kwa
kuonesha mifano kadha wa kadha, wakati wa kuzaliwa, wakati wa kufa, wakati wa
kupanda, wakati wa kuvuna n.k.
2Nyakati 1:7-10
Hapa tunamuona Sulemani anafanywa
mfalme, akaona hekima na maarifa aliyo nayo hayamtoshi, yalikuwa yanamtosha
wakati akiwa kijana, raia wa kawaida; ila wakati huu ni mfalme, hivyo akitazama
kazi aliyonayo na kiwango cha hekima na maarifa aliyonayo, haoni uwiano. Mungu
anamtokea na kumuuliza, "...omba lolote utakalo nikupe..." Mara
Sulemani akakumbuka kiwango chake cha hekima na maarifa wakati huo, akamwambia
Mungu, "...nipe sasa hekima na maarifa, nijue kuingia na kutoka mbele ya
watu hawa..." Nataka uone jambo hili mahali hapa, si kwamba Sulemani
hakuwa na hekima ama maarifa; alikuwa nayo, ila ya kujiongoza mwenyewe. Sasa
wakati huu amekuwa mfalme, hivyo anahitaji hekima na maarifa ya kuwaongoza watu
wengine.
Daniel 9:2,3
"...mimi Danieli, kwa kuvisoma
vitabu, nalitambua hesabu ya miaka, ambayo neno la Mungu lilimjia Yeremia
nabii, ya kutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani miaka sabini."
Daniel anaposoma kitabu cha nabii
Yeremia anatambua kuwa, wakati waliopo hawapaswi kuwepo Babeli, ila wanatakiwa
kuwa wameondoka. Kilichokuwa kimeendelea kuwaweka Babeli ni kutokujua nyakati
na majira ambayo wanatakiwa kuondoka Babeli.
Kwa hiyo baada ya Daniel kutambua kuwa
walipaswa kukaa Babeli kwa miaka sabini ndipo akamlilia Mungu kumweleza kwamba
wanatakiwa waondoke hapo. Kumbe kilichokuwa kinaendelea kuwaweka Babeli ni
kutokujua wakati.