SOMO:
TAMBUA NYAKATI NA MAJIRA
- UTANGULIZI.TAMBUA NYAKATI NA MAJIRA
Utangulizi
Hatima ya mwanadamu imefungwa katika
nyakati na Majira usipotambuwa wakati na majira ya Mungu juu ya Maisha yako
hilo ni tatizo
Tunapozungumza kwa habari ya nyakati na
majira tuna maana hii;
- Majira: Ni vipindi mbalimbali ndani ya wakati ulioamriwa; mfano masika, kipupwe, kiangazi, n.k
- Nyakati: Ni vipindi kulingana na matukio ya makusudi; mfano asubuhi, jioni, nyakati za mwisho, nyakati za utandawazi, wakati wa kupanda, kuvuna, n.k
Ni muhimu sana kufanya kila jambo kwa
wakati na majira yake, mfano kupanda wakati wa kupanda, kuvuna wakati wa
kuvuna, n.k
Siku zote ukifanya jambo nje ya wakati
wake utaonekana kituko, na matokeo yake ni kutokufanikiwa. Kila jambo huonekana
la busara mbele ya wenye hekima likifanyika ndani ya wakati wake, kwa lugha
nyingine, "Everything is right at right time". Maana yake ni kwamba
ukifanya jambo nje ya wakati hata kama jambo hilo ni jema, litabadilika kuwa
baya. Wakati una 'impact' kubwa sana katika jambo lolote. Tazama formula
ifuatayo;
- Luka 19:42 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.
- Kila jambo kuna majira yake na wakati wa kila kusudi,
“Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati wa
kila kusudi chini ya mbingu” (Muhubiri 3:1)
9,000,000 +Nyakati isiyo sahihi = 0
- Kitu sahihi +Muda usiyo sahihi = sifuri
Kitu sahihi +wakati sahihi= na Mazidisho
yaani mafanikio
Kwa hiyo unaweza kuona ni jinsi gani
wakati unavyoweza kuathiri mamboyako hii
ndiyo Kwa hiyo jambo ni jema sana likifanywa ndani ya muda wake. Kwa mfano,
tendo lile lile linalofanywa na wanandoa likifanywa na watu ambao si wanandoa
linakuwa si sahihi.
- Wala tendo halijabadilika, ni lile lile lakini kwa nini likifanywa na wanandoa ni sahihi na likifanywa na watu ambao si wanandoa sio sahihi? Tena limepewa na jina jingine kabisa, uzinzi; na ukifanya jehanamu unakwenda kwa miguu yote miwili. Tatizo hapa ni wakati!
Mhubiri 3:1-3
Hapa mwandishi anajaribu kutueleza kuwa
kila jambo lina wakati na majira yake, tena kila kusudi. Anasisitiza kwa
kuonesha mifano kadha wa kadha, wakati wa kuzaliwa, wakati wa kufa, wakati wa
kupanda, wakati wa kuvuna n.k.
2Nyakati 1:7-10
Hapa tunamuona Sulemani anafanywa
mfalme, akaona hekima na maarifa aliyo nayo hayamtoshi, yalikuwa yanamtosha
wakati akiwa kijana, raia wa kawaida; ila wakati huu ni mfalme, hivyo akitazama
kazi aliyonayo na kiwango cha hekima na maarifa aliyonayo, haoni uwiano. Mungu
anamtokea na kumuuliza, "...omba lolote utakalo nikupe..." Mara
Sulemani akakumbuka kiwango chake cha hekima na maarifa wakati huo, akamwambia
Mungu, "...nipe sasa hekima na maarifa, nijue kuingia na kutoka mbele ya
watu hawa..." Nataka uone jambo hili mahali hapa, si kwamba Sulemani
hakuwa na hekima ama maarifa; alikuwa nayo, ila ya kujiongoza mwenyewe. Sasa
wakati huu amekuwa mfalme, hivyo anahitaji hekima na maarifa ya kuwaongoza watu
wengine.
Daniel 9:2,3
"...mimi Danieli, kwa kuvisoma
vitabu, nalitambua hesabu ya miaka, ambayo neno la Mungu lilimjia Yeremia
nabii, ya kutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani miaka sabini."
Daniel anaposoma kitabu cha nabii
Yeremia anatambua kuwa, wakati waliopo hawapaswi kuwepo Babeli, ila wanatakiwa
kuwa wameondoka. Kilichokuwa kimeendelea kuwaweka Babeli ni kutokujua nyakati
na majira ambayo wanatakiwa kuondoka Babeli.
Kwa hiyo baada ya Daniel kutambua kuwa
walipaswa kukaa Babeli kwa miaka sabini ndipo akamlilia Mungu kumweleza kwamba
wanatakiwa waondoke hapo. Kumbe kilichokuwa kinaendelea kuwaweka Babeli ni
kutokujua wakati.
1 Nyakati 12:32
"Na wa wana wa Isakari , watu wenye
akili za kujua NYAKATI, kuyajua yawapasayo Israel wayatende; ... na ndugu zao
wote walikuwa chini ya amri yao"
Mungu alijua umuhimu wa watu wa namna
hii,watu wanaojua nyakati, kujua wakati gani Israel wanapaswa kufanya nini.
Tena Biblia inasema, kwa sababu tu ya wao kujua nyakati, "...ndugu zao
wote walikuwa chini ya amri yao". Kwa hiyo ukijua wakati gani unapaswa
kufanya nini, utakuwa na ujasiri wa kufanya mambo yako na siku zote utakuwa mtu
wa kufanikiwa. Hii ni kwa sababu kila jambo chini ya jua hufanyika ndani ya
wakati ulioamriwa, kulingana na mazingira husika. Na ndio maana leo ukikutana
na mtu na kumuuliza kwa nini unafanya unachokifanya atakwambia 'nakwenda na
wakati'. Ukijua ni wakati gani kitu gani kitatokea utajiandaa kukabiliana
nacho.
Mathayo 26:36-46
Yesu alipojua ama alipotambua wakati wa
kusulubiwa, alijiandaa kwa kufanya maombi mazito ya kuomba ujasiri wa
kukabiliana na hali halisi iliyopo. Kama unafikiri natania, kasome mwenyewe
utaona kuna wakati alisema "... kama ikiwezekana kikombe hiki
kiniepuke..." Kwa hiyo maombi aliyokuwa anayafanya, kwa kutambua wakati
alionao yalikuwa na umuhimu mkubwa sana, na ni kwa maombi hayo ndipo malaika
alishuka akamtia nguvu. Sasa fikiri kama asingejua kuwa huo ndio ulikuwa wakati
wa kusulubiwa, halafu asiende kuomba; unafikiri huyo malaika wa kumtia nguvu
ama moyo angempata wapi! Ukijua wakati gani unapaswa kufanya nini, utakaa
katika eneo husika na utajiandaa kukabiliana na jambo hilo.
Nimekupa dondoo hizo chache za Biblia
ili tu uone ni jinsi gani ni muhimu kujua na kutambua nyakati na majira
unayoishi.
Nikueleze tu kwamba mafanikio yako ya
kiroho na kimwili huendana sana na wakati. Watu hatufanikiwi kwa sababu tu
hatujui ni zama gani tunazoishi sasa na tunapaswa kufanya nini. Kwa mfano,
kipindi Yesu yuko duniani, yaani karne ya kwanza AD, ilikuwa mtu akiwa na gari
linalovutwa na punda, ndiyo alikuwa anaitwa amefanikiwa, ama kwa maneno mengine
yeye ni tajiri! Lakini mtu huyo huyo kwa kipindi chetu tunachoishi sasa si
tajiri tena kwani mikokoteni ya kuvutwa na punda ni kwa ajili ya kukatia majani
ya ng'ombe, kuchotea maji maeneo yenye ukame, kubebea samaki kwa wavuvi,
kuzolea takataka kwa maeneo ya mjini, tena uswahilini,n.k. Mafanikio ni yale
yale, lakini wakati! Kimsingi kabisa, kinachofanyika leo si kitakachofanyika
kesho.
ili zikusaidie kufikiri na kutenda ki –
muda. Biblia katika Mwanzo 18:14 inasema “Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda
BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata
mwana wa kiume”
Kushikilia
Ahadi ya Mungu,
Je umeshawahi kufikiri kwa nini ilibidi
Mungu aweke wazi muda wa Sara kumzalia Ibrahimu mtoto? Mungu alitaka Ibrahimu
atumie taarifa aliyopewa si tu kuifunga/kuiweka imani yake kwenye ahadi
aliyopewa bali zaidi kupata alichokitarajia ndani ya muda maalum aliosema Mungu
juu yao. Hivyo ni muhimu ujifunze kukishikilia kwa imani na mombi kile ambacho
Mungu amekusudia kukitenda juu yako kwa nyakati husika.
Mwanzo
18:14 katika bibilia ya kiingereza inasema “Is anything too hard for the LORD? At the
appointed time I will return to you, about this time next year, and Sarah shall
have a son.” Umeona neno hili “appointed time” naam ni lazima ujue kwamba
kwenye kila jambo linalopaswa kufanyika kufuatana na kusudi lako hapa duniani
kuna ‘appointed time”.Unapotamkiwa neno la kinabii na Mtumishi wa Mungu ukaambiwa
muda wa jambo kutokea ni wewe kusubiri
matokeo
Mungu
si mwanadamu akasema Uongo,
Hesabu
23:19Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si
mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza? Tazama,
nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua.
Kumbuka appointed time yako katika mambo
yako mbalimbali ni tofauti kabisa na ile ya watu wengine. Hivyo kadri
unavyokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu nyakati na kushirikiana nazo ndivyo
unavyoweka mazingira ya kuhakikisha appointed time yako inakuwa halisi kwa
kuzaa kilichotarajiwa. Hivyo ni muhimu
sana si tu uwe na ufahamu wa kutosha wa nyakati bali zaidi sana ujue namna ya
kushirikiana na hizo nyakati maishani mwako.
Tujifunze
kutoka kwa Lea mkewe Yakobo
Katika Mwanzo 29:31 Biblia inasema ‘Lea akapata mimba, akazaa mwana,
akampa jina lake Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa BWANA ameona teso langu; sasa
Mungu wangu atanipenda’
Wewe kama ni msomaji wa Biblia utagundua
kwamba haikuwa mapenzi ya Yakobo kumuoa Lea bali Raheli. Na kwa sababu hiyo
upendo wa Yakobo kwa Lea haukuwa mkubwa sana (Mwanzo 29:30). Maandiko yanasema BWANA Mwenyewe akaona kwamba Lea
hakupendwa ndipo akalifungua tumbo la Lea akaanza kuzaa watoto.
Naam Lea alijua na alimaanisha kwamba
hata kama mume wangu alikuwa na sababu ya kutonipenda, kitendo cha Mungu
kufungua tumbo langu na kuzaliwa kwa Reubeni ni appointed time ya kwangu ambayo
inazaa upendo wa mume wangu kwangu. Naam jambo la msingi ilikuwa si kuzaliwa
Reubeni bali ilikuwa ni kile ambacho Ruebeni anakileta yaani kuzaliwa kwa
upendo kwenye ndoa ya Lea na Yakobo.
Tujifunze kutoka kwa wana wa Israeli
Hesabu
9:22 – 23 inasema ‘Ikiwa lile wingu lilikawia,
likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka wana wa Israeli walikaa
katika kambi yao wasisafiri’. Bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya BWANA
walipiga kambi yao, na kwa amri ya BWANA walisafiri; wakayalinda malinzi ya
BWANA, kwa mkono wa Musa’. Naam andiko hili linatuonyesha kwamba BWANA ndiye
aliyekuwa akiamua muda wa kila jambo juu ya wana wa Israeli naam muda wa
kusafiri na muda wa kutulia maskani kwa ishara ya wingu. Ndiyo kwa kila muda
kulikuwa kuna vitu ambavyo Mungu alikuwa anavifanya kwa watu wake.
Katika Zaburi 32:8 Biblia inasema “Nitakufundisha na kukuonyesha njia
utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu, likikutazama’. Maandiko haya mawili
yanatupa kujua kwamba ili nyakati zilizoamriwa na Mungu juu yako ziweze
kuzaa/kuachilia/kufunua kile kilichofichwa/kilichobebwa/kilichohifadhiwa ndani
yake sharti mwanadamu ajifunze kumtumia Roho Mtakatifu kama kiongozi wa maisha
yake hapa duniani.
Tujifunze kutoka kwenye ufuno wa Yohana
kuhusu Ibilisi
Biblia katika Ufunuo waYohana 12:13 inasema ‘… Ole wa nchi na
bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye gadhabu nyingi, akijua ya
kuwa ana wakati mchache tu’. Tafakari
hivi, endapo Ibilisi anajua kwamba ana muda mchache tu, uwe na uhakika
amejipanga kuutumia vizuri ili kuhakikisha malengo yake yanatimizwa kwa
asilimia mia moja ndani ya muda mchache uliosalia.
Naam ili malengo yake yasifanikiwe juu
yako, kwenye familia yako, kanisa lako, nchi yako nk. ni muhimu sana wana wa
Mungu si tu wakajua nini mapenzi ya Mungu wao kwa nyakati alizoweka juu yao
bali zaidi sana wadumu katika kuyatenda. Naam jambo hili limesisitizwa pia na
Mzee wetu Petro aliposema ‘Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za
wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa
duniani” (1Petro 4:2)
Tujifunze kupitia Yezebeli
Ufunuo
2: 21“Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki
kuutubia uzinzi wake’. Je umeona jambo hili, hapa Yesu alikuwa akisema na
Kanisa la Thiatira kuhusu kujiepusha na Yezebeli mwanamke ambaye alikuwa
analiharibu kanisa hilo. Licha ya makosa yake Mungu akatoa muda wa Yezebeli
kutubu wala hakutaka kutubia uovu wake. Na ni muhimu utambue kwamba muda
aliopewa Yezebeli kutubu ulikuwa na kikomo.
Hata leo bado Mungu anatoa muda na fursa
nyingi sana za watu wake kutubu na kutengeneza njia zao. Ile kwamba mwenzi
wako, watoto wako, ndugu zako wanaendelea kuishi hata kama ni watenda maovu
haina maana kwamba Mungu anafurahia uovu wao au haoni. Fahamu kwamba kimya
chake ni muda ambao anautoa kwa wanadamu kutubu na kumrudia kwa kuwa yeye
hafurahii kifo cha mwenye dhambi. Naam muda aliouweka juu yako, nyumba yako nk
kutubu ukipita na walengwa wakakataa mabaya zaidi yatatokea kama ilivyokuwa kwa
Yezebeli, miji ya Sodoma na Gomora nk.
Hivyo kwa kuwa wewe umepata ufahamu huu
ni vema ukajifunza kushirikiana na muda wa kutubu ambao Mungu ameachilia juu
yako, familia yako, kanisa lako, taifa lako nk, ili kwa njia ya maombi yako
uiponye nyumba yako na Taifa lako pia.
Tujifunze kupitia Paulo na Timotheo
Biblia katika 2Timotheo4:2 inasema ‘Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na
wakati usikokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho’.
Katika maneno haya tunajifunza kwamba kumbe kwa kila jambo kuna wakati unaofaa
na usiofaa.
Jambo muhimu kwako ni kuwa tayari
kuyatenda mapenzi ya Mungu kwa kila kipindi uanchopitia maishani mwako ili
ndani ya vipindi husika yatimie yale yaliyokusudiwa na Mungu kutimia. Na hii ni
kutokana na ukweli kwamba nyakati zimeamriwa na Mungu, kutoa ushirikiano kwa
mtu ambaye anazingatia maagizo ya Mungu na sheria zake.
Naam ningeweza kuendelea kukuonyesha
maandiko mengine kadhaa ndani ya Biblia lakini ninapomaliza natamani kusisitiza
kuhusu kuwaombea wale waliopewa kuwa na akili za kujua nyakati zinazokuhusu
katika ngazi mbalimbali. Ukirejea1Mambo
ya
Nyakati 12:32 Biblia inasema “Na wana wa Isakari, watu wenye akili za
kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao vilikuwa watu
mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao”
Kutokana na andiko hili, ni dhahiri
kwamba si watu wote waliopewa akili za kujua nyakati za yale yanayokuja ili
kuwaongoza wengine namna ya kuyakabili. Hata hivyo uwe na uhakika kwamba
kutokana na umuhimu wa jambo hili Mungu ameweka katika kila familia, kanisa,
Taasisi, Taifa nk watu ambao ndani yao kuna akili za kujua nyakati zinazohusu
familia, kanisa , taasisi au taifa husika ili wawasaidie wengine kujua
yawapasayo kutenda kwa kila nyakati.
Hivyo ni muhimu sana ukajifunza
kuwaombea watu wa namna hiyo kwenye familia yenu, kanisa, taifa nk kwa kuwa
ndani yao kuna nyakati zote ambazo unapaswa/mnapaswa kuzipitia. Naam ni muhimu
sana kuwaombea ili mosi wajitambue na pili wakae kwenye nafasi zao kwa kuwa
ndani yao Mungu si tu ameweka akili za kujua nyakati bali zaidi namna ya
kufanya katika kila nyakati zinazokuja juu yako.
Nami nakushukuru, Baba, Mungu wa wote
wenye mwili, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia
watoto wachanga
Hitimisho:
Mhubiri 7:14 Isaya 44:26