KUBOMOA MISINGI MIBOVU
Maisha halisi tuliyopaswa kuishi
Manzo 1:26, Yakobo 4:7, Zaburi 103:3
Baba Nabii Akifundisha jinsi ya kubomoa misingi Mibovu iliyojengwa na Muovu shetani katika ufahamu wa wanawa Mungu. pale Hema ya kinabii ibada za katikati ya wiki
Msingi halisi wa Mungu
Imeandikwa mwanzo 1:26 Ndipo Mungu
akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki
wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya
viumbe wote watambaao juu ya nchi.’’ Kwa hiyo Mungu alimwumba mtu kwa mfano
wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanaume na mwanamke aliwaumba.
Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke,
mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani
na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.’’
Baada ya ya Dunia kukamilika katika
uumbaji wa Mungu katika viumbe wote kiumbe mmoja tu ndiye aliyepewa upendeleo
wa kipekee kabisa kwaajili ya Mungu kuimarisha ufalme wake duniani kupitia
kiumbe huyo ‘’Mwanadamu’’ Mungu alitaka mwanadamu aishi kwa kumwamini tu, Mungu
hakumuwekea mwanadamu sharia ya kumkandamiza Zaidi alimpendelea sana
‘’Mbambo sita aliyopendelewa Mwanadamu na Mungu,’’Mwanzo
1:26
v
Mwanadamu ni mfano wa Mungu mwenyewe
kwaajili ya ufalme wake
v
Muonekano wa Mwanadamu umebeba sura
ya Mungu
v
Mwanadamu amepewa umiliki wa Dunia na
kilichopo ndani yake
v
Mwanadamu amepewa nguvu ya Zaidi na
utiisho juu ya viumbe wengine wote, inchi kavu,baharini, angani,
v
Mwanadamu ameberikiwa tangu kuumbwa
kwake, kwaajili ya ongezeko
v
Mwanadamu amepewa Utisho wakipekee…
‘’Uharibifu wa kwanza juu ya Msingi
uliyokuwa umejengwa na Mungu umeanzia hapa’’
Imeandikwa Mwanzo 3:1-5 Basi nyoka
alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao BWANA Mungu aliowafanya.
Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya
mti wo wote wa bustanini?’ ’’ 2Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda
ya miti iliyoko bustanini, 3lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti
ulio katikati ya bustani, wala msiguse kabisa, la sivyo mtakufa.’ ’’
4Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa. 5Kwa
maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala macho yenu yatafumbuliwa, nanyi
mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.’’
Sababu za Anguko la Mwanadamu
lilisababishwa na nini mifano michache, Yakob 4:7
v
Alimuasi Mungu kwa kutokutii agizo
walilipewa
v
Mwanadamu hakuwa tayari kumpinga
shetani,
v
Adui alikuwa Mwerevu sana kuliko
viumbe wengine adui alikuwa na ‘’ufahamu mkubwa’’
v
Mwanamke hakumtii Mungu kwasababu ya
ushawishi wa adui
v
Adui alihakikisha amebomoa mahusiano
mema yaliyokuwa yamejengwa baina ya mwanadamu na Mungu,
v
dui aliwabadilishia maagizo ya
kufuata shetani akataka fafuate maagizo yake,
v
Adui anabomoa msingi uliowekwa na
Mungu kwamba watakapofanya kinyume watakufa, ila kwasababu ya uharibifu
uliofanywa na kujengewa msingi mubovu bado hawakuogopa kifo,
v
Eve kilicho mvutia na kumpendeza
moyoni ni kutokufa, kufunguliwa macho,na kuwa kama Mungu
v
Eva alitoa nafasi ya kumsikiliza Adui
Imeandikwa Mpingeni shetani naye atawakimbia,
Swali je Msingi halisi uliojengwa na Mungu ndani yako
ukiutafuta bado unauona? Jibu unalo wewe Adui mahali anakowatesa watu sana ni
katika Ufahamu wao anawabadilishia taarifa kutoka katika uhalisia kwenda kwenye
ubovu,
Mawazo ya Mungu kwetu na mikakati aliliyoihaidi ni ipi? Yeremia
29:11
Mungu anatuwazia mawazo yaliyomema wakati wote,na muovu
anatuwazia mabaya wakati wote imeandikwa
Yeremia 29:11 maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,’’ asema
BWANA. “Ni mipango ya kuwafanikisha
na wala si ya kuwadhuru, ni mipango
ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. 12Kisha mtaniita na mtakuja na kuniomba,
nami nitawasikiliza. 13Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu
wote. 14Nitaonekana kwenu,” asema BWANA, “nami nitawarudisha watu wenu
waliotekwa. Nitawakusanya kutoka katika mataifa yote
Maumivu mateso maangaiko yote
tunayopitia yanatoka wapi? Zaburi 103:3
Unaporudishiwa maisha yako hatua yakwanza nikusamehewa juu ya
misingi mibovu aliyokuwa ameijenga muovu, Mungu hataki kutuona na hali kama hii
tunayoishi maisha ya kuacha uhalisia na kuishi maisha bandia Mungu
anavyokuangalia kule muovu anakupeleka anajisikia vibaya sana
Muovu ni baba wa giza na mambo yake anayafanyia gizani hiyo
ndiyo sababu anadanganya na kuwaibia kirahisi maana watu hawaoni imeandikwa Mariko 8:18 wana macho ila hawaoni
wanamasikio hayasikii, Tumeibiwa vitu vingi sana
Afya imeibiwa,akili za watoto,Amani katika
jamii,mali,biashara,kazi vyote vimeibiwa vinatakiwa virudishwe imeandikwa
hapana arudishae imeandikwa Isaya 42:22 watu
wameibiwa hata wao wamefichwa mashimoni, wao na mali zao luka 12:34 hazina ya Mtu alipo ndipo yeye
alipo
,imeandikwa yohana 10:10 Mwivi
huja ili aibe, kuua na kuangamiza. ‘’Yesu Kristo’’Mimi nimekuja ili wapate
uzima kisha wawe nao tele.
‘‘Mimi ndimi Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema huutoa uhai
Wake kwa ajili ya kondoo.
Kinacho watesa watu wa Mungu ni nini?
Ni misingi mibovu
Imeandikwa Hosea 4;6 Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa
Maarifa, “Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami
nitakukataa wewe usiwe
Kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu
wako mimi nami sitawajali watoto wako. Imeandikwa
mithali 1:7 Kumcha BWANA ndiyo chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu
hudharau hekima na adabu, na kumcha Mungu ni kushika
o
Kumcha Mungu ni kusikia sauti yake na kuiamini
o
Kumcha Mungu ni kushika neno lake Mungu
o
Kumcha Mungu ni Kulitendea kazi Neno lake bila kuongeza au
kupinguza
Kupunguzwa au kuongezwa kwa Neno la
Mungu huo ndio tunauita msingi mbovu
Kazi kubwa ya Muovu shetani nia kuharibu Msingi wa Neno la
Mungu na kujenga Msingi wake wa uharibifu, anachokifanya yeye ni kuhakikisha
wanadamu aliyependelewa na Mungu namna hiyo anatakiwa kukosana na Mungu ili
Kumuondolea nguvu Mwanadamu, aliyekuwa amekabithiwa kila kitu katika hii Dunia,
Imeandikwa Warumi 6:21-26 Lakini sasa, haki itokayo kwa Mungu
imedhihirishwa pasipo sheria, ambayo Torati na Manabii wanaishuhudia. Haki hii
itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio. Kwa maana hapo hakuna tofauti, kwa kuwa wote wametenda
dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wanahesabiwa haki bure kwa neema
Yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. Yeye ambaye Mungu alimtoa
awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu Yake. Alifanya hivi ili
kuonyesha haki Yake, kwa sababu kwa ustahimili Wake aliziachilia zile dhambi
zilizotangulia kufanywa. Alifanya hivyo ili kuonyesha haki Yake wakati huu, ili
Yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Yesu.
Unapomwamini Yesu kristo kuwa bwana na Mwukozi wa Maisha
yako jambo kubwa linalifanyika –unakuwa umehamishwa kutoka ufalme flani kuwa
ufalme mpya imeandikwa wakolosai 1:13 Kwa
maana alituokoa kutoka katika ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa
Mwana Wake mpendwa, 14ambaye katika Yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu
yake, yaani, msamaha wa dhambi.
Kuhamishwa Ni tendo la kiroho unaweza
usione na macho haya ya damu na nyama imeandikwa mariko 8:18 wana macho ila
hawaoni wana masikio ila haysikii na akili haikumbuki,
v
Kumwamini Yesu ni kuhama kutoka Imani
ya awali na kuingia katika Imani mpya
nikukubali msingi mubovu uharibike na ujengwe mpya, wa kumwamini yeye
kwa moyo wako wote
v
Kumwamini Yesu kristo siyo kuiamini
Dini bali ni kiona njia ya kweli ya
kwenda katika ufalme wa Mungu na kuifuata
v
Kumwamini yesu ni kurudisha maisha
yako halisi anayoyataka Mungu uyaishi
v
Kumwamini Yesu ni kusajiriwa katika
kitabu cha uzima wa milele
v
Kumwamini yesu ni kupata kitambulisho
halali cha kutumia jina la Yesu katika maombi yako
v
Kumwamini yesu unamaanisha kukubali
kusamehewa dhambi zako zote
v
Kumwamini yesu unakubali udhamani wa
Damu iliyomwagika pale msalabani
v
Kumwamini yesu ni kuanza maisha ya
Umilele
Yote haya ni baada ya wewe kukubali yote yaliyofichwa na
muovu kufichuliwa kwaajili ya wewe kuwa huru kabisa imeandikwa ili uwe huru
kutoka katika vifungo unachohitaji ni kitu kimoja yaani kweli ya kristo imeandikwa Yohana 8;18 Mtaifahamu Kweli
na hiyo kweli itawaweka huru kweli kweli,
Watu wanahitaji kweli siyo mambo
mengine na neno la Mungu kwakuwa neno ni Mungu mwenyewe,
Imeandikwa Yohana 1:1 Hapo mwanzo,
alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.
Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna cho
chote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima na huo
uzima ulikuwa nuru ya watu. 5Nuru hung’aa gizani nalo giza halikuishinda.
Hili neno tunaloliongea sasa ndani
yake kuna nguvu ya Mungu, ya kutenda mambo yote,
Maandiko yanauwa bali neno linahuwisha:
Mateso ya watu wengi yanatokana na kile walichofundishwa
na kuaminishwa kuwa ndicho sahihi na msaada pekee,kumbe si kweli yale watu
waliyojifunza kwa wazazi tangu utoto wao kile walichojifunza kwa jamii
iliyowazungu, walichojifunza mashuleni walichojifunza katika umaja kama vyama
au dini,
Neno la Mungu linaweka wazi kuwa maandiko yanauwa bali
neno linauhusha .Maandiko ni yale maandishi unayoyasoma Katika bibilia ila Neno
ni ule uhalisia wa ile nguvu iliyo ndani ya maandishi,
Mfano,sharia ikitungwa ikiwekwa kwenye maandishi, unafanya
kazi kulingana na nguvu inayosaidia ile sharia ifanye kazai, seria ni utaratibu
ambao yeyete anayependa kuishi kwa utaratibu anaweza akaweka sharia zake hata
katika familia zipo sharia nyingi zimewekwa na wazazi japo hazikuandikwa, na
zinafuatwe wangeweza kuziandikwa na zikafanya kazi tu,
Sasa kama seria ikiwekwa na ukaifahamu na usiifuate
itakutawala, na ndiyo maana sharia zinawatesa sana wavunja sharia,
Kwamfano: wakitunga sharia ya walevi kutokunywa pombe
watakaoteswa na sharia ni walevi wa pombe kwaambaye hatumii haimuhusu, ndiyo
sababu Yesu aliona sharia zinawatesa wakina Munsa akaja ili watu waishi kwa
Neema ya Neno la Mungu yaani Yesu akaye ndani Yao,
v
Chunguza
maisha yako:
v
Haya mateso
chanzo chake kimetoka wapi,
v
Je kile
unachokuamini kimekusaidia namna gani
v
Imani yako
msaada ni upi
v
Jamii
iliyokuzunguka mchango wake au msaada wake ni upi
v
Ndugu
wanakusaidia vipi katika hali unayopitia?
Chochote ulichokiamini kama ni msaada au ni kitu chema
kikashindwa kukusaidia,iwe ni mtu au kitu,jamaa,rafiki wakaribu .msomi mmoja aliwahi kusema heri mtu mmoja
anayekusaidia wakati wa shida kuliko watu 1000 wanaokushangilia wakati wa
furaha,