Powered By Blogger

Monday, 2 March 2015

VITA KATIKA ULIMWENGU WA KIROHO



       SOMO: VITA KATIKA ULIMWENGU WA KIROHO

 

 










 Utangulizi,Vita ni Mapambano,baina ya pande mbili,  mapambano ya aina yeyote yanatambulika kama ni vita, sasa mapambano hayo yanategemeana na ni yananmna gani na yanafanyika katika mazingira yapi kama kulivyo na tofauti ya vita ndivyo ilivyo mazingira ya vita na namna ya vita leo sisi tunajifunza vita katika ulimwengu wa kiroho Yaani mapambano yanayofanyika katika Ulimwengu Usioonekana kwa macho Haya ya kawaida, ni hadi uwe na macho ya ki-roho,

                                      Mambo ya kufahamu katika vita vya Kiroho
  • Mtambuwe adui yako kabla hujaingia katika vita
  • Tambuwa uwezo na Nguvu aliyonayo adui yako
  • Ni vema kama inawezekana ukafahamu na Mbinu anazozitumia
  •  fahamu Unapigana vita vya namna gani
  • Pambana vita vya Ushindi na siyokushindwa
  •  Pima silaha zako zinatosha kuanzisha vita na kumaliza
  • Tambua uwezo na mamlaka iliyo upande wako,
Efeso 6:10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.   Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.  Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.  Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
  • Baada yakutambuwa na kufahamu vita katika ulimwengu wa kiroho,
Ukishasema ni mapambano basi fanya mapambano achana na mizaha,2timoth 2:4?hakuna apigae vita ajitiae katiaka shughuli za dunia 7 Mungu hakutupaIsaya 49:24 je aliye hodari aweza kupokonywa mateka yake
  • Wakikusanyana wataanguka wote

Isaya 54:14 Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia.   Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.
Namna unavyoongezeka katika kulijuwa Neno La Mungu ndivyo ujasiri na  nguvu yako ya kupambana inazidi, kuongezeka Efeso 3:20 kwa kadri ya nguvu itendayo kazi {neno li hai tena lina nguvu}
  • Siku ya Matatizo Hutakiwi kuzimia
Mithali 24:10   Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.
  Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. Hainamaana Ukiona mtu anauwawa au anauwa unaanza kupambana  kumbuka vita ya Ibilisi anaaza kuipigia katika Ulimwengu wa kiroho, mazara ni matokeo ya matukio aliyoyasababisha katika ulimwengu wa kiroho,
  • Silaha zetu ni kuangusha Ngome ,mawazo na kila kitu kiinukacho,
2kor 10:3  Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;  (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)  tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
Ayubu 22:28 nawe utakusudia neno nalo litathibitka kwako
Kiri kwa kinywa chako sasa Kuangusha kila ngome zilizo jengwa juu ya maisha yako,familia,uchumba ,biashara kwa jina la Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai angusha Ngome ya ibilisi sasa,
  • Kila kitakachovaa umbo lolote angusha chini,
Luka 10:19 nimewapa amri ya kukanyaga inge na nyoka na nguvu zote za yule adui
  • Angusha Nguvu  zote siyo nusu  Ngu ya mauiti,magonjwa,umasikini,hasira,uwoga,kukataliwa,kuharibikiwa, ianguke katika jina la Yesu
  • Mungu anaangalia ninani aliyetarari kupambana 
Ezekieli 22:30 nami nikatafuta mtu miongoni mwao {atakayepigana atakaye fight sikuona}
Zab 91:13 utawakanyaga samba na nyoka, mwanasimba na joka utawaseta chini ya miguu
  • Muovu shetani anakutafuta akumeze kama sima anavyokula nyama, yeye ni mwivi wa afya, mali nk.. anakushitaki kwa Mungu kwa makosa anayokusababishia yeye mwenyewe, lazima apigwe leo,na ngome yake kusabaratishwa katika maisha yetu,
1petro 5:8 mshitaki wenu kama samba anazunguka akitafuta mtu ammeze
Yoh 10:10 mwivi haji ila aibe na kuharibu mimi nalikuja ili wawe na uzima kasha wawe nao tele
Sasa leo zamu yake kupata hasara katika imaya yake katika ufalme wake,
Yer 11:10 nimekuweka juu ya mataifa na juu ya falme ili kungoa na kuharibu kujenga na kupanda

Yakobo 4:7mpingeni shetani nae atawakimbia
Efeso 4:21-32 msimpe ibilisi nafasi,
Huwezi kuingiakwa mwenye nguvu pasipo kumfunga ili kuviteka vitu vyake
Sasa umeshaelewa kumbe kuna vita vya kiroho vinaendelea juu ya maisha yako, Hapo kazini,hapo nyumbani vita vya kiroho vinafanyika kwaajili yako maisha yangu hapo shuleni,hapo chuoni,ukiwa barabarani juwa kuwa kunavita vinapamba moto juu ya maisha yako, kwa jina la Yesu innasambalatisha kila maadui juu ya maisha yako sema Amina kuwa tena,
Mungu akubariki kushiriki ujumbe huu, endelea kuwa nasi kipindi kijacho, somo lijalo ni muendelezo wa somo hili hili ila pia ikiwa unahitaji ushauri au maombezi Zaidi, unaruhusiwa kupiga simu kwa Mtu wa Mungu Nabii Samson au unaweza ukaja pale hema ya kinabii nyankumbu-Bonde la Uzima, piga simu sasa Huduma hii ni Bure
                                             
                                            0756 809209

BE BLESSED


Ninawezaje Pata amani?

Unawezaje kupata amani? Baba Nabii akifunua siri ya kuwa na amani kama ya kwake aliyonayo Utangulizi kazi kubwa kabisa kwa Mwanadamu...