Powered By Blogger

Wednesday, 17 June 2015

MGUSO


MGUSO WA NENO LA MUNGU



Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya

Ndani ya Hema ya kinabii Bonde la uzima Nyankumbu Tanzania

UTANGULIZI: 


Ujumbe huu ni ujumbe ambao waweza kubadilisha maisha yako kama utaamua kufungua moyo wako, kwasababu mwenendo wa maisha waweza kukufanya uhisi kuwa hakuna matumaini lakini leo baada ya kufutilia  somo hili uwezekano wa Maisha yako kubadilika ni mkubwa sana naamini hivyo katika jina la Yesu sema amina……

Kila Neno la Mungu lina pumzi hai mtaji wako ni kuamini , muone Mtumishi wa Mungu hapa Ezekeli ,

Ezekieli 37:11 "kisha akaniambia, mwanadamu mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli tazama wao husema mifupa yetu imekauka matumaini yetu yametupotea, tumekatiliwa mbali kabisa" 

Ukiendelea kufuatilia kwa karibu kwa habari ya Ezekieli utagundua sababu ya Mungu kumleta katika bonde lile lililojaa mifupa. Kwanza, Imani ya Ezekieli ilikuwa imani yenye matumaini. Ingawa hali halisi ya mifupa ilikuwa imekwisha kauka, yeye alibaki na tumaini kuwa mifupa ile yaweza kuishi.


Hatua kubwa sana ya kudhihirisha kuwa mtu anamjua Mungu, ni ile ambayo mtu mmoja katikati ya vita, au hali za kukatisha tamaa, au hana analolitegemea katika maisha yake lakini bado anataja mambo yajayo, anataja matendo makuu ya Mungu anamwamini na kumtumaini Mungu

Ninawezaje Pata amani?

Unawezaje kupata amani? Baba Nabii akifunua siri ya kuwa na amani kama ya kwake aliyonayo Utangulizi kazi kubwa kabisa kwa Mwanadamu...