MGUSO WA NENO LA MUNGU
Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya
Ndani ya Hema ya kinabii Bonde la uzima Nyankumbu Tanzania
UTANGULIZI:
Ujumbe huu ni
ujumbe ambao waweza kubadilisha maisha yako kama utaamua kufungua moyo wako,
kwasababu mwenendo wa maisha waweza kukufanya uhisi kuwa hakuna matumaini
lakini leo baada ya kufutilia somo hili uwezekano
wa Maisha yako kubadilika ni mkubwa sana naamini hivyo katika jina la Yesu sema
amina……
Kila Neno la
Mungu lina pumzi hai mtaji wako ni kuamini , muone Mtumishi wa Mungu hapa
Ezekeli ,
Ezekieli
37:11 "kisha akaniambia, mwanadamu mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli
tazama wao husema mifupa yetu imekauka matumaini yetu yametupotea, tumekatiliwa
mbali kabisa"
Ukiendelea
kufuatilia kwa karibu kwa habari ya Ezekieli utagundua sababu ya Mungu kumleta
katika bonde lile lililojaa mifupa. Kwanza, Imani ya Ezekieli ilikuwa imani
yenye matumaini. Ingawa hali halisi ya mifupa ilikuwa imekwisha kauka, yeye
alibaki na tumaini kuwa mifupa ile yaweza kuishi.
Hatua kubwa
sana ya kudhihirisha kuwa mtu anamjua Mungu, ni ile ambayo mtu mmoja katikati
ya vita, au hali za kukatisha tamaa, au hana analolitegemea katika maisha yake
lakini bado anataja mambo yajayo, anataja matendo makuu ya Mungu anamwamini na
kumtumaini Mungu
Mungu hapendi
ukate tamaa, wala umkufuru yeye katikati ya magumu na kwa taarifa yako tu ni
kuwa watu wakubwa katika biblia hata walioitwa na Mungu, walipitia magumu sana lakini katikati ya magumu hayo walitamka
maneno ya ushindi. Pia, kutamka maneno ya matumaini katikati ya magumu
kunakufanya utoke mapema kwenye hali mtu aliyokoau anayopitia
Inawezekana
unapitia katika hali ngumu kwa sasa, lakini utakalolinena ukiwa katika dhiki
hiyo itakufanya ama utoke ukiwa shujaa au aliyeshindwa. Na ndio maana hata
Ezekieli alipowekwa mbele ya mifupa mikavu na kuulizwa 'je mifupa hiyo yaweza
kuishi?' Naye alijibu kuwa 'wewe Bwana wajua', akionyesha kuwa hakuna jambo la
kumshinda Bwana. Na ndio maana hata alipopewa nafasi ya kutamka neno alitamka
uzima. Ni muhimu kujua maneno ya kutamka pindi unapopitia katika hali ngumu.
Ni muhimu
kujua unachokiongea leo ndicho utakachokiishi kesho na maandiko yanajifunua
kwetu tutashiba matunda ya kinywa chetu isijishibishe sumu itakayokumaliza pole
pole wengine hujikuta wanaongea maneno mabaya juu yao wenyewe, huku wakisahau
kuwa ni shetani ambaye anawafanya waongee maneno hayo ili apate nafasi ya
kuharibu maisha yao baadaye.
Isaya 57:10 "ulikuwa umechoka kwaajili ya
urefu wa njia yako, lakini hukusema hapana matumaini, ulipata kuuhishwa nguvu
zako, kwasababu hiyo hukuugua" kumbe watu hawa, hali yao halisi iliwafanya
wakate tamaa ya kufika wanapokwenda lakini pamoja na urefu wa njia bado
walikiri kuwa matumaini yapo. Na kwasababu ya ukiri huo walipewa nguvu mpya.
Usikiri udhaifu, Mungu anayetenda miujiza yupo na ukimkimbilia yeye, ataiondoa
aibu yako na kukuvika kicheko.
Ukifuatilia
habari ya Yusufu ambaye maisha yake yalianza kwa kuuzwa na ndugu zake kwa
wamisri. Na alipouzwa waliigawa kanzu yake maana yake aliuzwa bila mavazi,
lakini akiwa Misri na matumaini yakaanza kuja likatokea jambo jingine la
kukatisha tamaa. Mke wa potifa akamsingizia kuwa anataka kumbaka, hivyo
akatupwa gerezani maisha katiaka hali hiyo ni dhahiri kuwa Yusufu alikata tamaa
kabisa. Lakini alipotoka gerezani Yusufu akawa waziri mkuu, jiulize, Mungu
aliyemfanya kuwa waziri mkuu alikuwa wapi kipindi anauzwa? Au jiulize alikuwa
wapi kipindi anawekwa gerezani? Anasingiziwa kubakwa Ruhusu kusudi la
Mungu lifanyike katika maisha yako
Ni muhimu
kujua kuwa sio kuwa kwa unayopitia hali ngumu ukahisi Mungu amekuacha, si
kweli; Mungu bado yupo pamoja na wewe na matumaini bado yapo. Yesu Kristo ni
tumaini la kutosha kwenye maisha yako. Leo sikia sauti yake hii ikisema. Pata
muda kuingia kwenye maombi na Mungu anakupa tumaini jipya leo. Inawezekana
unapitia shida za ndoa, matatizo kazini, vita shuleni, huduma ni ngumu watumishi wengine wamekuinukia roho ya kukataliwa mpaka umejihisi hakuna
kesho ile uliyoiwaza jana Leo tambua
kuwa hata Ayubu katikati ya dhiki kuu hakuwahi kumkufuru Mungu Niko ambaye niko
jina lake bali aliweka tumaini lake
kwake na kwa saa sahihi matumaini makuu yalionekana.Tunajifunza kwao maana
walishinda swali ushindi wako uko wapi? Ili
wengine wapate shule ya kujifunza?
Hata kama
ndoto yako inaonekana inataka kuzimika, inawezekana ulikuwa na ndoto za kusoma
katika maisha yako lakini sasa unaona muda umeenda nakwambia bado lipo tumaini.
Inawezekana madktari walikwambia kuwa mwisho wa kuzaa ni miaka 45 na wewe sasa
unajiona unaelekea huo umri ukiwa hauna mtoto;unmechumbiwa na wanaume wengi
hakuna anayekamilisha Harusi kiasi sasa unahisi aibu kwa jamii, umechelewa
kuoa unahisi kuwa uko na mikosi usiogope Mungu bado yopo kwaajili yako na
anakupenda kuliko mwanadamu yeyote yule uliyewahi kumfahamu lakini nakwambia neno ambalo Yesu amenituma
kwalo kuwa USIKATE TAMAA