MGUSO WA NENO LA MUNGU
Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya
Ndani ya Hema ya kinabii Bonde la uzima Nyankumbu Tanzania
UTANGULIZI:
Ujumbe huu ni
ujumbe ambao waweza kubadilisha maisha yako kama utaamua kufungua moyo wako,
kwasababu mwenendo wa maisha waweza kukufanya uhisi kuwa hakuna matumaini
lakini leo baada ya kufutilia somo hili uwezekano
wa Maisha yako kubadilika ni mkubwa sana naamini hivyo katika jina la Yesu sema
amina……
Kila Neno la
Mungu lina pumzi hai mtaji wako ni kuamini , muone Mtumishi wa Mungu hapa
Ezekeli ,
Ezekieli
37:11 "kisha akaniambia, mwanadamu mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli
tazama wao husema mifupa yetu imekauka matumaini yetu yametupotea, tumekatiliwa
mbali kabisa"
Ukiendelea
kufuatilia kwa karibu kwa habari ya Ezekieli utagundua sababu ya Mungu kumleta
katika bonde lile lililojaa mifupa. Kwanza, Imani ya Ezekieli ilikuwa imani
yenye matumaini. Ingawa hali halisi ya mifupa ilikuwa imekwisha kauka, yeye
alibaki na tumaini kuwa mifupa ile yaweza kuishi.
Hatua kubwa
sana ya kudhihirisha kuwa mtu anamjua Mungu, ni ile ambayo mtu mmoja katikati
ya vita, au hali za kukatisha tamaa, au hana analolitegemea katika maisha yake
lakini bado anataja mambo yajayo, anataja matendo makuu ya Mungu anamwamini na
kumtumaini Mungu