Powered By Blogger

Wednesday, 28 March 2018

Ninawezaje Pata amani?

Unawezaje kupata amani?

BONDE LA UZIMA GEITA
Baba Nabii akifunua siri ya kuwa na amani kama ya kwake aliyonayo


Utangulizi
kazi kubwa kabisa kwa Mwanadamu Ni namna ya kuishi maisha ya amani, familia inatafuta amani kwa wazazi,wazazi nao wanaitafuta kwakufanya kila wanaloliweza imeshindikana,wanandoa walikimbilia katika ndoa wakifikiri amani inaishi ndani ya ndoa leao wanajuuta, namna pekee ya kupata mani ni kuwa na Mahusiano mazuri na Mungu

Unajiuliza swali Naweza kupata amani vipi? Imeandikwa Ayubu 22:21 "Mjue sana Mungu ili mwena amani ndivyo mema yatakavyokujia."

Amani nikufanya mambo yako kuwa sawa na Mungu au kuwana uhusiano mwema na Mungu. Imeandikwa, Warumi 5:1 "Basi tukisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani na mwe na amani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu kristo."
Amani ni zawadi kutoka kwa Mungu. Imeandikwa, Yohana 14:27 "Imani na waachieni, amani yangu na wapa niwapovyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo msifadhaike mioyoni mwenu wala msiwe na woga."

Amani huja kwa njia ya kuzitii amri za Mungu. Imeandikwa, Zaburi 119:165 "Wana amani nyingi waipendao sheria yako wala hawna la kuwakwaza."
Nivema kuwa na nia ya kutafuta amani. Imeandikwa, Warumi 14:19. "Basi kama ni hivyo na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana."
Amani ni ngao. Imeandikwa, Zaburi 122:6-7 "Utakieni Yerusalemu amani na wafanikiwe

wakupendao amani na ikaendani ya kuta zako."
Je nawezaje kuiweka amani ambayo nimeipata?. Imeandikwa, Isaya 26:3-4 "Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu kwa kuwa anakutumaini mtumaini Bwana siku zote maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele."
Furaha huja kwa kuw na mapatano mema na watu. Imeandikwa, Mathayo 5:9 "Heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu."

Unayopenda kutendewa na wewe tendea wengine

Unapotendewa ubaya na Adui ufanye Nini

BONDE LA UZIMA GEITA
Utangulizi:
mara nyingi watu wanapenda vitu vizuri watendewe na wengine ila wao wenyewe hawako tayari kuwatenendea mazuri wengine .kabla hujasema kwanini mimi jiulize na wewe umefanya nini kwa mwingine?



Tunapaswa kuwa tendea vipi maadui wetu? imeandikwa Luka 6:27-36 "Lakini nawaambia ninyi mnaosikia wapendeni adui zenu watendeeni mema wele ambao wawachukia ninyi wabarikieni wale ambao wawalani ninyi waombeeni wale ambao waonea ninyi akupigae shavu moja mgeuzie lapili naye akunyang'anyaye joho lako usimzuilie na kanzu mpe kila akuombaye na akunyag'anyaye vitu vyako, 

usitake akurudishie nakama mnavyo taka watu wawatendee ninyi watendeeni vivyo hivyo
Maana mkiwapenda wele wawapendao ninyi mwaonyesha fadhili gani? kwa kuwa hata wenye dhambi wawapenda wale wawapendao nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema mwaonyesha fadhili gani? hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. Na mkiwakopesha watu vitu huku mkitumaini kupata kitu kwao mwaonyesha fadhili gani? hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi ili warudishiwe vile vile basi wapendeni adui zenu tendeni mema na kukopesha msitumaini kupata malipo na dhawabu yenu itakuwa nyingi nanyi mtakuwa wana wa aliye juu kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasio mshukuru na weovu basi iweni na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma."
Tuwatendee maadui zetu kwa roho njema. Imeadikwa Mathayo 5:25 "Patana na mshitaki wako upesi wakati uwapo pamoja naye njiani yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi na kadhi akakupeleka kwa askari ukatupwa gerzani."
Usifurahi katika majonzi ya adui zako. Imeandikwa Medhali 24:17-18 "Usifurahi adui yako aangukapo; wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; Bwana asije akaliona hilo likamkasirisha akgeuzia mbali naye hasira yake."
Imeandikwa Warumi 12:20 "Lakini adui yako akiwa na njaa mlishe akiwa na kiu mnyeweshe maana ufanyapo hivyo utampalia makaa ya moto kichwani pake."
Mungu ametuahidi kutuhifadhi kutokana na maanui wetu imeandikwa Zaburi 18:48 "Hutniponya na adui zangu naam waniinua juu yao walioniinukia na kuniponya na mtu wa jeuri." 

Sheria haiwezi kuwa kuu kuliko Neema,

BONDE LA UZIMA GEITA

Imani ikikosa matendo ni sawa na mtu aliyeaga kwenda safari ila bado ameketi alafu anasema safari si muda mrefu atafika ikiwa bado yupo pale pale, chukuwa tendo la kusonga mbele juu ya kile unachokiamini,

Matendo Bila Imani


Matendo bila imani ni hali ya kuweka sheria kuwa ya muhimu kuliko Mungu na mahitaji ya watu. je unaamini kwa matendo au kwa kinywa tu? Imeandikwa, Mathayo 12:9-10 "akaondoka huka akaingia katika sinagogi lao na tazama yumo mtu mwenye mkono umepooza wakamuuliza wakisema ni halali kuponya watu siku ya Sabato? wapate kumshitaki akawaaambia ni mtu yupi miongoni mwenu kondoo mmoja na yule koondo ametumbukia

shimoni siku ya Sabato asiyemshika akamwopoa?."
Matendo bila imani ni sawa na utumwa. imeandikwa, Wagalatia 4:8-9 "Lakini wakati ule kwa kuwa hamkumjua Mungu mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu bali sasa mkisha kumjua Mungu au zaidi kujulikana na Mungu kwa nini kuyarejea tena mafundisho mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge yenye upungufu ambayo mnataka kuyatumikia tena mnashika siku za miezi na nyakati na miaka."

Matendo bila imani huvutia lakini huharibu. Imeandikwa, Wakolosai 2:23 "Mambo hayo yana onekana kana kwamba yana hekima katika namna ya ibada mliyo jitungia wenyewe na katika kunyenyekea na katika kuutawala mwili kwa ukali lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili."
Tunaokolewa kwa imani bali si kwa matendo.

Imeandikwa, Waefeso 2:8-10 "Kwa maana mmeokolewa kwa neema kwa njia ya imani abayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa cha Mungu wala si kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu, maana tu kazi yake tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo."

imani inahitaji matendo

Matendo Bila Imani


BONDE LA UZIMA GEITA
Utangulizi:
Matendo bila imani ni hali ya kuweka sheria kuwa ya muhimu kuliko Mungu na mahiji ya watu. Imeandikwa, Mathayo 12:9-10 "akaondoka huka akaingia katika sinagogi lao na tazama yumo mtu mwenye mkono umepooza wakamuuliza wakisema ni halali kuponya watu siku ya Sabato? wapate kumshitaki akawaaambia ni mtu yupi miongoni mwenu kondoo mmoja na yule koondo ametumbukia shimoni siku ya Sabato asiyemshika akamwopoa?."
Matendo bila imani ni sawa na utumwa. imeandikwa, Wagalatia 4:8-9 "Lakini wakati ule kwa kuwa hamkumjua Mungu mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu bali sasa mkisha kumjua Mungu au zaidi kujulikana na Mungu kwa nini kuyarejea tena mafundisho mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge yenye upungufu ambayo mnataka kuyatumikia tena mnashika siku za miezi na nyakati na miaka."
Matendo bila imani huvutia lakini huharibu. Imeandikwa, Wakolosai 2:23 "Mambo hayo yana onekana kana kwamba yana hekima katika namna ya ibada mliyo jitungia wenyewe na katika kunyenyekea na katika kuutawala mwili kwa ukali lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili."
Tunaokolewa kwa imani bali si kwa matendo. Imeandikwa, Waefeso 2:8-10 "Kwa maana mmeokolewa kwa neema kwa njia ya imani abayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa cha Mungu wala si kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu, maana tu kazi yake tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo." 

Maisha ya mwenye haki -Nabii Samson Mboya


KITUO CHA PILI – DARASA LA MJUMBE 
Na Baba Nabii Samson Mboya 
MAISHA YA USHINDI -IMANI
BONDE LA UZIMA GEITA
Utangulizi:ili kuishi Maisha ya ushindi unahitaji kuwa na imani kuu juu ya ushindi uliyopata kutoka Ka Mungu, uliyemwamini,
Imeandikwa waebrania 10:38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.
Kumbe haki ya mwana wa Mungu inapatikana kwanjia ya imani
v Mwenye haki wa Mungu ataishi  kwa kumwamini Mungu
v Akisali anamwamini Mungu ameshajibu Maombi yake Imeandikwa Isaya 65:24 kabla ya kuoamba nitajibu ukiwa katika kunena nitasikia,
v Lazima fikira zako uziamini juu ya kile unachokiwaza
v Lazima maamuzi yako uyaamini bila mashaka
v Lazima msimamo wako uuamini kuwa hukukosea kumwamini Yesu
v Lazima ujiamini hata wewe mwenyewe kwamba uko katika njia sahihi ya Mungu mwenyewe
v Lazima uamini ulipomwamini Yesu kristo kuwa bwana kuwa bana na muokozi wa maisha yako uliingia katika ufalme mpya
v Lazima uamini uhamisho wako ulifanyika kweli na uamini maisha mapya ya ufalme wa nuru imeandikwako wakolosai 1:13 nayealituhamisha kutoka katika ufalme wa giza,
v Kuwa na mashaka juu ya imani yako kwa Mungu ni chukizo kwa Mungu,
v Lazima uamini kwa tangu ulipomwamini Yesu wewe ulihamishwa kwenye wasiwasi,mashaka huzuni,mateso magonjwa maisha machafu ni mwiko kwako sasa,
v Maisha ya imani yanafaida kwa na ushindi usiyowa kawaida, maana hakuna cha kukutisha kwa namna yeyote,
Imani nini? Imeandikwa waebrania 11:1 "Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana." Imani nikuwa na uwakika ya juu ya kile kitu unachokitarajia kuwa nacho au kikipata katika maisha yako ambacho kwa wakati huo hakipo mikononi bali unakitarajia kukiona na kukichukuwa,
Yesu ndiye mwanzo wa imani imeandikwa Luka 17:5 "Mitume wakamwambia Bwana tuongezee imani."Imeandikwa Warumi 10:17 yasema "Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo."
Imani ya haki ni kuamini yote ambayo Yesu ametutendea. imeandikwa Warumi 5:1 "Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na imani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu kristo."
Imani ni kuwa na hakika juu ya ahadi zote za Mungu alizoziahidi Imani ni kuwana imani kwa Mungu katika mambo yote. imeandikwa Waebrania 10:38 "Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani naye akisita-sita Roho yangu haina furaha naye."
Imani dhaifu yaweza kuwa yenye nguvu Mungu akimsaidia mtu imeandikwa Marko 9:24 "Mara babaye yule kijana akapaza sauti akasema Naamini nisaidie kutokuamini kwangu."  Kumbe unaweza kusaidiwa na Mungu katika kutokuamini kwako,

Friday, 16 March 2018

Kazi ya watumishi wa Mungu ni kuinena kweli ya Mungu basi,

EPUKA WEZI WA  MAWAZO
Utangulizi:
Kihualisia Mungu ametoa upendeleo  kwa kila  mwanadamu awe na kichwa chake japo kuna watu wanatumia vichwa vyao na bado wanataka watumie na vichwa vya watu wengine, Mungu amefanya hivyo ili kila mmoja aweze kuwaza na kuamua juu ya maisha anayoyataka,

Sasa kuna watu ambao mimi nawapa jina la wezi wa mawazo ya watu, wao wanataka kile wanachokiwaza kionekane ni saghihi hatakama si sahihi ilimradi wao wanaona vile wanavyo ona basi  wanalazimisha wengine waone hivyo ikiwezekana hata katika vitendo wafanye kama wanavyotaka au kupenda wao hilo naliita wizi wa mawazo iwe kwa ushawishi au kwa kupewa zawadi huo ni wizi wa mawazo,

Katika maisha Mungu amekuwekea muelekeo wako kwaajili ya kufanikiwa  soma bibilia yako wana waizraeli walipitishwa katikati ya bahari si kwamba walipenda ila ilitakiwa wapite hapo kwaajili ya kufika kule walikotakiwa kwenda, 

Tatizo lolote linalokuandama usilikimbize kwa watu mpelekee Mungu Huruma za watu ni za muda mfupi sana leo ukipata tatizo watakuja na watakuonyesha machozi kama wako pamoja na wewe siku tatu tu wamesahau maumivu unabaki nayo wewe kama wewe,

wakati mwingine  wanakuliwaza kumbe ndiyo hao hao wanaosababisha maumivu yako imeandikwa mathayo 10:36 na Adui za Mtu ni wale wa nyumbani kwake, si kila mtu anayekuonyesha anakupenda ni kweli yuko upande wako.

Tumia akili yako kuishi maisha unayoyapenda  tumia akili yako jifunze kwa watu maamuzi na vitendo jitahidi viwe vya kwako usiishi kwakupangiwa maisha unayotakiwa kuishi wewe kama wewe,

kuwa makini,jiepushe na wezi wa mawazo,hao wanapatikana kila mahali,katika mabasi,masokoni,katika majumba ya ibada,katika mitandao, wanachezea akili yako usikubali kufuata kitu usichokitaka katika maisha yako, kila unalolifanya jiulize mara tano linafaida kwa nani,linafaida kwalini,kwanini ufanye .

Wednesday, 14 March 2018

Mnara wa mateso

Imeandikwa mwanzo 11:1-9
Watu wakajenga mnara kwenda mbinguni,kama walimjengea Mungu mnara je, watu haohao watashindwa kukujengea na wewe? Kuna watu wanaishi katika mateso maana wamejengewa minara ya madeni, magonjwa,shida ,mikosi ,balaa na shida mbalimbali, .Kumbe Kuna mnara unaowatesa  .
Imeandikwa mwanzo 1:26
Mungu akasema na tumfanye mtu kwa sura yetu namfono wetu akaijaze nchi .lakini watu wakamuasi Mungu kwa kutofuata maelekezo,  wakajikusanya na kujijengea mnara ili kujijengea heshima ya majina yao.
Unapoteseka adui yako anafurahia sana.wanakaa vikao na kushauriana ,wakujengee mnara wa aina gani, mnara wa magonjwa,kukataliwa, madeni, au kuvunja ndoa. Vikao vyao wanajua wanapovifanyia,Ni vikao vyao kiroho huwezi kuviona  kwa macho ya kawaida .Na huwa Wana maeneo maalumu ya kufanyia vikao hivyo.
Ili uweze kuwashinda na kuwachafulia lugha unahitaji msaada wa Mungu kupitia maombi ya kuchafua lugha zao na kubomoa hiyo minara.

Muongozo wa Maisha ya mwanadamu-katiba ya Mungu ni- Bibilia







Jibu la maswali yako ni Neno la Mungu
1: Biblia ni neno timilifu la Mungu, linalo ongoza kwa Roho Mtakatifu, na lina kila jibu la matatizo ya mwanadamu. (2 Timotheo 3:16-17 na 2 Petro 1:20-21).

2: Kuna Mungu mmoja , aliye katika namna tatu : Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. (Yohana 10:30 , Yohana 14:26 na Wafilipi 2:5-7).

3: Mungu ni pendo na anapenda watu wote. Ni shauku yake kufikia watu ambao ni maskini , waliodhulumiwa,walio wajane au yatima, na kuponya waliovunjika mioyo .(Zaburi 68:5 - 6 na 1 Yohana 4:16).

4: Mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu lakini dhambi imemtenga na Mungu. Bila Yesu hatuwezi kuwa na uhusiano na Mungu.(Mwanzo 1:26 na 1 Timotheo 2:05).

5: Tunaweza kuwa na uhusiano binafsi na Mungu kwa njia ya wokovu, karama ya bure ya Mungu kwa mwanadamu. Sio matokeo ya ambacho tunakifanya, ila tu inapatikana kwa msaada wa bure wa Mungu. Kwa kukiri tumetenda dhambi na kuamini katika kufa, kuzikwa, na kufufuka kwa Kristo , na kumkubali Yeye kama Bwana , tunaweza kuwa na Mungu milele. (Waefeso 2:8 - 9 ; Warumi 5:1 na Warumi 3:24)

6: Tunaamini katika ubatizo wa maji , kama ilivyofundishwa na kuoneshwa na Yesu, kama njia kwa ajili ya waaminio kutambua kwa kufa, kuzikwa, na kufufuka kwa Yesu. (Mathayo 28:19; Warumi 6:04 and Mathayo 3:13-17).

7: Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni zawadi kutoka kwa Mungu. Husaidia kumwezesha muumini kuendeleza tabia ya Kristo na kuishi kila siku katika mapenzi ya Mungu. (Mathayo 3:11 and Matendo 2:04).

8: Mungu huwapa wote waaminio karama za kiroho. Wao ni kwa ajili ya kuimarisha watu wa Mungu ( Kanisa) na kuthibitisha uwepo na nguvu za Mungu kwa wasioamini. Zawadi ya Roho ni hai na ni muhimu inayohusika leo ​​. ( 1 Petro 41 Wakorintho 12:4-11 and:10).

9: Utakaso ni mchakato unaoendelea wa kuruhusu tabia ya Mungu kukuwa ndani yetu. (Warumi 6:19 na Wagalatia 5:22-25).

10: Uponyaji wa Mungu ni hai katika maisha ya leo kupitia Yesu Kristo, ambaye ni Mponyaji. Uponyaji ni pamoja na kimwili, kiakili, kihisia na mrejesho wa kiroho. (Luka 9:11; Mathayo 9:35; Matendo 10:38 na Mathayo 10:1).

11: Biblia inaeleza kuzimu kama mahali halisi. Ni mahali pa mateso na mahali pa kujitenga kabisa na Mungu kwa wale wanao kufa bila ya kumkubali Kristo. Shahuku ya Mungu ni kwamba hakuna atakayetengwa na yeye milele , ndiyo maana alimtuma Mwana wake , Yesu Kristo, duniani. (Waebrania 9:27 , Ufunuo 20:12-15 na Yohana 3:16-18).

12: Yesu atarudi na kuchukua waliompokea kama Mwokozi kuwa pamoja naye milele. (Matendo 1:11 , 1 Wathesalonike 4:13-17 na Waebrania 9:28).




Ninawezaje Pata amani?

Unawezaje kupata amani? Baba Nabii akifunua siri ya kuwa na amani kama ya kwake aliyonayo Utangulizi kazi kubwa kabisa kwa Mwanadamu...