NAMNA YA KUING’OA ROHO YA UHARIBIFU
Utanguli: kila jambo
linalofanyika chini ya jua lazima lina chanzo chake, na kila tatizo linalotokea
katika maisha yako lina chanzo, Angalia chanzo cha Tatizo usiangalie mwanzo wa
tatizo,
Mungu ametupatia nafasi ya kujifunza Namna ya kushugulikia chanzo cha
tatizo na siyo mwanzo wa tatizo, usipomjua adui na uwezo alio nao si rahisi
kupambana naye
Kufanikiwa au kushindwa kwa jambo lolote lazima kuwepo na nguvu ya
kusababisha matokeo ya matarajio, inatoka Roho ya Uharibibu katika maisha yetu,
Yeremia 1:10, Mathayo 15:13
Mungu huongea nasi kupitia neno lake, Roho Mtakatifu, na neno lake
ni chakula cha roho zetu, hivyo haitoshi kujua neno la Mungu pekee bila kuwa
nalo miyoyoni mwetu na neno kuwa sehemu ya miyoyo yetu.
“Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya
Mlima” - (Mathayo 5:14).
Wewe na mimi tuliumbwa kuangazwa na nuru yake ulimwenguni. Kama
watoto wake tunaweza kuchukua nuru na matumaini katika ulimwengu wetu.
Hatupaswi kuficha nuru yetu, lakini badala yake ni lazima kuangaza. Hivyo,
angaza, angaza na endelea kuangaza.
Tafuta
Chanzo na Siyo Mwanzo.
Kujua mwanzo wa tatizo pekee bila kujua chanzo chake, haitoshi
kutatua tatizo, hivyo yatupasa kusimama katika imani na kuacha Roho wa Mungu
kutuongoza katika kila jambo..
ROHO YA UHARIBIFU NI NINI?
Roho ya Uharibifu ni Nguvu inayotenda kazi kupitia umbo flani,
na inaitwa roho ya uharibifu kwakuwa kazi yake ni kuharibu Mtu,mali,vitu,yaani
Hii roho kwa luga nyingine tunaweza kuiita fundi mkuu katika karakana ya shetani, kwakuwa yeye ni
kutengeneza matatizo tu, mauti, kukosa
kazi, kutoolewa,kuoa, kuzaa mapoza, kuna magonjwa, kuna umaskini, kukataliwa.
2WAFALME 2:19 “watu wa mjini wakamwambia
Elisha, angalia twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri kama bwana wangu
aonavyo, lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapoza”. Unaweza ukawa
unafanya biashara Fulani na unaweza ukawa unapata faida lakini kumbe ndani ya
biashara hiyo kuna mauti. Kwa mfano: biashara ya bodaboda, watu wanasema
“asante mchina ametusaidia” lakini
angalia jinsi ambavyo watu wengi wanakufa kutokana na hizo bodaboda.
LUKA 19: 41-43 “ Alipofika karibu aliuona
mji, akaulilia akisema laity ungalijua yata wewe katika siku hii yapasayo
amani, lakini sasa yamefichwa machoni pako………….”
Hapa Bwana Yesu aliuona ule
mji na akawa anaona mauti ndani ya huo mji lakini watu wengine walijua ni amani
walizidi kushangilia na kufurahi (mstari
wa 37)
lakini mafarisayo waliona wivu na walijua kuwa wao na mji wao wako
salama hata hawamwitaji Yesu. Hivyo walianza kuwanyamazisha wanafunzi wa Yesu.
Bwana Yesu aliwajibu kuwa wajaponyamaza wanafunzi hawa, mawe yatainuka na
kushangilia hivyo hivyo. Huu mji wa yerusalemu Bwana Yesu aliuona uharibifu
uliokuwa mbele yake na ndivyo ulivyo mji wa uharibifu umejaa damu japokuwa mtu
huwezi ukauona kwa macho.
NAHUMU 3:1-4 “Ole wake mji wa damu, umejaa mambo ya uongo
na unyang’anyi, mateka hayaondoki…….. kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa Yule
kahaba mzuri, Yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na
jamaa za watu kwa uchawi wake. Kwenye vijiji utakuta kuna mtu mmoja ambaya ni
mchawi na kila mtu anajua kabisa kuwa huyo mtu ni mchawi lakini wanamwogopa
kijiji kizima wanamwogopa kwa ajili ya mambo yake ya uchawi. Hivyo kupitia yeye
mji mzima umejaa damu kwa ajili ya kuwaua watu lakini hiyo miji yote ni lazima
iharibiwe kwa Jina la Yesu.
Katika mahubiri yaho mchungaji alizidi
kusisitiza kuwa ni muhimu kufahamu kuwa kuna maisha ambayo watu wanayaishi ni
maisha magumu yamejaa taabu ambazo hata kama rais wan chi angeamua kukussaidia
asingeweza. Kwa mfano kama mtu umechukuliwa msukule, rais wan chi hawezi
kukutoa msukuleni, yeye atakachoweza kufanya atahakikisha kuleta huduma za
jamii mfano kujenga shule, kuleta umeme, kuleta maji, lakini rais wa nchi
hawezi kukusaidia wewe ukiwa unakandamizwa na wachawi, ni mpaka pale ambapo
watu wote watakapoamua kumtegemea Yesu ndipo watakapoweza kuwekwa huru mbali na
mji wa mauti. Hivyo ni muhimu kufahamu kuwa miji ya mauti inaweza kupanga vifo
kwa ajili ya watu, lakini kwa wale ambao ni wana wa ufufuo mji wa mauti hauna
nguvu juu yao.