Powered By Blogger

Wednesday, 14 March 2018

MIKUTANO YA INJILI YA MTAA KWA MTAA



Baba Nabii akimshukuru Mungu Kwaajili ya kuanza kuhutumia katika mkutano wa mtaa




Utangulizi … 

ROHO WA BWANA YUKO JUU YANGU AMENIPAKA MAFUTA
Luka 4:18 ………………….Roho wa bwana yu juu yangu amenipaka mafuta  kuwafunguwa wote waliofungwa na kuwatangazia mwaka wa bwana,
JINSI UNAVYOWEZA KUIBIWA NA UKATESWA BILA WEWE KUJUWA,
SIKU YA KWAZA,  Isaya  42:22 ……..watu hawa wameibiwa wamekuwa mawindo wamenaswa katika mashimo katika magereza,
KUYATAMBUA MASHIMO ULIYOCHIMBIWA NA ADUI  NA KUTOKA KWA NJIA YA MAOMBI

SIKU YA PILI 

 ZABURI 35:7… [Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi 
YEREMIA 5:26………. [Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu. 27 Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. 28 Wamewanda sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji. 29 Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema Bwana; na nafsi yangu

Namna ya kufungua kamba ulizofungwa na adui katikamaisha yako

SIKU YA TATU
 MATHAYO 10:36, ADUI YA MTU NI WANYUMBANI KWAKE
 ZABURI 140:5……..[Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi.]… Kwenye hili  andiko yapo mambo manne yaliyokaa kwa mtindo wa kamba: Mtego, kamba, wavu na matanzi. Kamba iitwayo ‘tanzi’ ni ile ya kusababisha kifo. Ndiyo maana watu wanaojinyonga, hutumia tanzi kwenye shingo zao. Hizi zote ni kamba zitokazo shimoni (kuzimu). Njia iliyoandikwa hapa siyo njia zako za 

kutembelea hapa duniani. Ni ile njia ya kuelekea kwenye mafanikio yako, kwenye njia ya kuelekea kuolewakwako, kwenye njia ya kufungua mradi wako, kwenye  njia ya Baraka zako. Katika njia hiyo, wapo watu wanaoweka mitego, tanzi, kamba, wavu na tanzi ili mtu asifikie mwisho wa hatima yake.


Ninawezaje Pata amani?

Unawezaje kupata amani? Baba Nabii akifunua siri ya kuwa na amani kama ya kwake aliyonayo Utangulizi kazi kubwa kabisa kwa Mwanadamu...