TUNAWEZAJE KUJENGA MISINGI IMARA
Baba nabii Samson Mboya akiendeleza somo la Namna ya kubomoa misingi Mibovu kwa wakamilifu waliyoudhuria ibada hiyo alinukuliwa akisema Muovu anawatesa watu kwa sababu wamekosa ufahamu wa Mungu imeandikwa Hosea 4:6 watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa watu wanachotakiwa kutafuta ni maarifa ya Mungu basi Maana bila hivyo hakuna usalama Dunia nzima inaumwa na wanaoishi ndani yake ni mautihuti wanahitaji msaada wa Mungu Mwenyewe
Yakobo 4:7, Mwanzo 1:26, Zaburi 103:3 Waibrania 10:32
Imeandikwa Yakobo 4:7 Basi mtiini
Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 8Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia
ninyi. Itakaseni mikono yenu, ninyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu,
ninyi wenye nia mbili. 9Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu na
kigeuzwe kuwa kuombeleza na furaha yenu kuwa huzuni. 10Jinyenyekezeni mbele za
Bwana, naye atawainua.
ü
Ili kujena misingi mipya baada ya kubomoa misingi mibovu unatakiwa
kumtii Mungu kwa kila agizo analokuagiza kupitia sauti yake kumbu 28:1
utakapoisikia sauti ya bwana Mungu wako,
ü
Kwanzia sasa Unatakiwa kumpinga
shetani,kila analokuletea,mawazo,moyoni,kupitia marafiki,ndugu mazingira
imeandikwa Mathayo 10:36,
ü
Kujenga misingi mibovu tunatakiwa
kurudisha mahusiano ya kweli kwa kuonyesha upendo mkuu juu ya neno la Mungu, imeandikwa Marko 12: 29 Yesu akajibu, “Amri iliyo kuu ndiyo hii, ‘Sikiza Ee
Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Mpende Bwana Mungu wako kwa
moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako
zote.’
ü
Tunajenga
mingi mpya kwa kuanza kuonyesha upendo mkuu mbele za Mungu kwaajili ya
kurudishiwa nafasi tuliyokuwa tumipoteza awali,
ü
Pamoja na uasi na kupoteza nafasi
kubwa tuliyokuwa tumepewa bado kwa upendo
Kuna Gharama za kulipa ili kujenga
misingi iliyobomolewa Mungu aligaramika mara ya pili kurudisha misingi mipya,
ili kumrudishia mwanadamu Heshima aliyokuwa ameipoteza,
Imeandikwa Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu
aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe
kuuhukumu ulimwengu, bali kwa Yeye ulimwengu upate kuokolewa.
Ye yote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa,
kwa sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu. Hii ndiyo hukumu kwamba: Nuru
imekuja ulimwenguni, nao watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao
ni maovu.
Kwa kuwa kila atendaye maovu huchukia nuru, wala haji kwenye nuru ili
matendo yake maovu yasifichuliwe.
Mungu anatufundisha nini hapa:
Mungu anatuonyesha kusudi kuu la
kumuumba mwanadamu, ilikuwa ni upendo wake kama vilile wazazi wanapokubaliana
kuowana na kujenga familia wanayoipenda,
Mungu anatuanyesha moyo wa utoaji
mkuu si kazi nyepesi kumtoa motto awe sadaka,
hili aliliweza Ibrahimu kwa Neema aliyopewa Na Mungu
Mungu hataki hata mtu mmoja apotee
hii inaonyesha jinsi mtu mmoja alivyo wa dhamani kubwa
Mungu anatuonyesha maishi yetu halisi
ni ya uzima wa milele na siyo yauhai tu,
Mungu anatufundisha tusipomwamini
tayari tumejikamilishia hukumu zetu wenyewe
Mungu anatuonyesha nuru yake ye neno
lake japo wengine wanakataa nuru, ikiwa hata wadudu wanaipenda nuru ukiwasha
taa gizani wanakimbilia,
Mungu anatuanyesha kilichotupeleka
tulikokuwa ni uovu na namna ulivyo mubaya
Ilikujenga msingi iliyoharibiwa na
Muovu katika maisha yako unahitaji machache yafuatayo
v
Upendo unahitajika
v
Imani inahitajika
v
Utiifu wa juu unahitajika
v
Tumaini kunahitajika
v
Uaminifu unahitajika
Haya ndiyo yatakayorudisha yaliyokuwa
yamepotea …….Yohana 15:14
v
Sura ya Mungu
v
Mfano wa Mungu
v
Kutawala kila kilicho chini ya jua
kwa Nguvu za Mungu
v
Kuwa na maamuzi ya ki Mungu
v
Kuishi kwa Amani ya Mungu
v
Kuishi kwa Kumtumaini Mungu,
Hakika wewe umependwa sana na tayari
umesha hamishwa katika Dunia ya mateso haupo
gizani tena maisha yako sasa si ya
kutazama bali ni yakuona katika ulimwengu wa Kiroho ukiishi kwa njia ya Imani
kila unalolitaka waibrania 10:38 mwenye haki ataishi kwa Imani…
**************************************************************************
MISINGI MIBOVU SEHEMU YA TATU
AWALI MAISHA YAKO YALIVYO KUWA
Umepata neema kubwa Sana kuifahamu kweli ya Mungu na ndiyo
msaada pekee kwake yeye aaminiye Imeandikwa
yohana 8:32 Ndipo mtaijua kweli nayo
kweli itawaweka huru.’’ Karibu wewe sasa uko huru na utaanza kuona na
kuhisi mabadiliko makubwa sana katika maisha yako hata marafiki ndugu jamaa
iliyokuzunguka wataanza kushuhudia hili Umeshaifahamu kweli na ndiyo hiyo
iliyokuweka huru kabisa na kukuhamisha toka katika mateso mengi ya ufalme wa
giza
Imeandikwa wakolosai 1:13 Kwa maana alituokoa
kutoka katika ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana Wake mpendwa,ambaye
katika Yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu yake, yaani, msamaha wa dhambi.
Kwaili kweli uliyoifahamu ukaiamini imekupa uwezo na
uhalali wa kuitwa mwana wa Mungu aliye hai.si rahisi Shetani kukuzewea tena
maana umehama katika imaya yake, alikuruhusu usali, uimbe lakini akushikilie
Gizani sasa basi,
Ø
Imeandikwa
warumi 8:1 Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu Kwa wale walio
ndani ya Kristo Yesu, wale ambao hawaenendi Kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata
Roho. 2Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru
mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Imeandikwa Yohan 1:12 Bali wote
waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio
Jina Lake. Hawa watoto wamezaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mwili au kwa
mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.
Ø
Tumeahamishwa kutoka katika ufalme wa
mateso ya kila namna
Ø
Hatukuona biashara ya kufanya maana
tulikuwa gizani
Ø
Hatukuweza kuwoa maana tulikuwa
gizani
Ø
Hatukuolewa maana tulikuwa gizani
Ø
Hatukuweza kufanya kazi wala biashara
maana tulikuwa gizani
Ø
Hatukuweza kumtumikia Mungu kwamaana
tulikuwa gizani
Ø
Hatukuweza kubarikiwa kwakuwa
tulikuwa gizani
Ø
Hatukuweza kutunza familia zetu
kwasababu tulikuwa gizani
Ø
Hatukuweza kuonyesha upendo wetu kwa
ndugu,jamaa na Marafiki maana tulikuwa gizani,
Ø
Hatukufurahia upendo wa Mungu kwakuwa
tulikuwa gizani
Ø
Tulikuwa na roho za kukataliwa maana
tulikuwa gizani
Ø
Hatukuwa na heshima wala muelekeo
kwakuwa tulikuwa gizani
Umeokolewa kwa Damu ya yesu yote yaliyokuwa yapepotea
yamerudi mara dufu kwa jina la Yesu Kristo.
Haya yote uliyakosa kwakuishi katika ufalme wa Giza
kwakuwa umemaanisha kuishi katika ufalme mpya wa pendo la Mungu tarajia mara
dufu yote yaliyokuwa yamepotea gezani, msingi kwako ni kudumu sana katika
kupata ufahamu mpya na maelekezo mapya kutoka kwa Mungu wako, Neno la Mungu
liko wazi kabisa.
Imeandikwa Wakolosai 2:6 Hivyo basi,
Kama vile mlivyompokea Kristo Yesu kuwa Bwana, endeleeni kukaa ndani Yake. Mwe
na mizizi, mkiwa mmejengwa ndani Yake, mkiimarishwa katika imani kama
mlivyofundishwa na kufurika kwa wingi wa shukrani.
Angalieni mtu ye yote asiwafanye ninyi mateka Kwa elimu
batili na madanganyo matupu yanayotegemea mapokeo ya wanadamu na mafundisho ya
ulimwengu ambayo siyo ya Kristo.
Maana ukamilifu wote wa uungu umo ndani ya Kristo katika
umbile la mwili wa kibinadamu, nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Kristo, ambaye
Yeye ndiye mkuu juu ya kila enzi na kila mamlaka.
Usiruhusu mashambulizi mapya juu ya
maisha yako mapya ya ufalme wa Mungu wa kweli
Imeandikwa Wakolosai 2:16 Kwa hiyo
mtu asiwahukumu ninyi kuhusu vyakula au vinywaji, au kuhusu kuadhimisha sikukuu
za dini, au Sikukuu za Mwandamo wa mwezi au Siku ya Sabato. Hizi zilikuwa
kivuli cha mambo ambayo yangekuja, lakini ile iliyo halisi imo ndani ya Kristo.
Simama imara katika Misingi ya Mungu
Adui hatochoka
kukufuatilia katika maisha yako anatafuta njia mpya ya kukurudisha katika Giza
na katika Kamba alizokuwa amekufunga kuwa makini na wala usitoe ruhusa kabia, imeandikwa
Yakobo 4:7 mtii Mungu Mpinge shetani nay eye atakukimbia, Umempata Yesu umepata
kila hitaji unalolitaka na si rahisi kujikwaa tena maana sasa katika hii Dunia
umepata taa imeandikwa Zaburi 119:105
"Neno lako ni taa ya miguu yangu Kumbe miguu
yako inahitaji taa ambalo ni neno la Mungu,
Shetani hatokuja Kama yeye bali atatuma wajumbe wake kuja
kukunyanyasa kwa maneno mabaya ya kukuumiza, ili urudi nyuma usikubali kata
kata, Shetani anaweza kutumia Mtu yeyeto kuyatesa maisha yako wewe mwenyewe ni
shahidi hapo ulikokuwa kuna watu wakaribu ndiyowaliyokuwa wametumika kuyatafuna
kuyatesa maisha yako imeandikwa Mathayo
10:36 na Adui za Mtu ni wale wa nyumbani kwake,
Kwanini shetani anapenda kutumia sana watu wa karibu ni
kwasababu wale watu wanakufahamu wewe kwa ukaribu sana ni rahisi kutumia
uenyeji wao kukukandandamiza chini kasha unakamatwa na kufunwa tena, na shetani akishakukamata mateso atayazidisha
mara mbili ya pale, wewe unafahamu
kwamba mfungwa akitoroka akikamatwa huwa anafanywa nini: anaongezewa kifungo
mara mbili ya awali.
Haki ya mkamilifu wa Mungu
inapatikana kwa kuamini kwa Moyo,
Imeandikwa Warumi 10; 10 Kwa maana
Kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na
hivyo kupata wokovu. 11Kama yasemavyo Maandiko, ‘‘ye yote amwaminiye
hatatahayarika.’
**************************************************************************
MISINGI MIBOVU SEHEMU YA NNE
MADHARA YA KURUDI NYUMA
Kwa kumwamini Yesu tayari wewe si wa kawaida tena wala
huwezekaniki na shetani tena Baraka ni haki yako kumb 28:1 kwa chochote
unachokitafuta sasa tafuta moyoni maana ndiko Mungu anaishi warumi 10:10 yote
ni kwaimani tu waibrania 11:6 lazima uamini Mungu aliyo ndani yako, Waefeso
3:20 nguvu zote ziko ndani yako, yohana 20:19 kuvuviwa nguvu na Mungu
huwezekaninki tena, luka 4:18
Madhara ya kurudi gizani
Iko wazi kabisa adui yako akifanikiwa
kukukamata na akapata nafasi ya kukufanyia ubaya atakufanyia mabaya kuliko yale
ya awali mfano: mfungwa akitoroka Gerezani akikamatwa huwa anaongezewa adhabu
ndivyo shetani akikukuta umerudi katika masikani yake, wewe ni shahidi hata
ukiwa na mfugo unaotoroka toroka siku ukijirudisha unafanya nini ni kuchinja au
kuuza kabisa, maana Adui anakuwa na wasiwasi kwamba kuna siku utatoroka tena,
Pepo anapotolewa ndani ya mtu aliyempagawa huondoka na baadae
hurudi na kuangalia kama anaweza kuingia tena.Ikiwa mtu huyo anaishi maisha ya dhambi huona
nyumba ni chafu na kuingia."
Imeandikwa luka 11:24 ‘’Pepo mchafu
amtokapo mtu, huzunguka zunguka sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa
kupumzika, lakini asipopata mahali po pote husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba
yangu nilikotoka.’ Arudipo na kuikuta ile nyumba imefagiliwa na kupambwa
vizuri, ndipo huenda na kuchukua pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye
mwenyewe, huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya
kuliko ile ya kwanza.’’
Mtu anapofunguliwa hatuwa ya kwanza anatakiwa umakini
mkubwa sana maana si kwamba adui anafurahia wewe kuwa mzima yeye alisha iba
mali zako akawa anazitumia maisha yako yalikuwa yanatumika na wale
aliyowaamulia wayatumie, mwili wako alishawapangisha wapangaji wasiyolipa kodi,
mali kazi biashara zote akaziharibu familia, kizazi chako akakipeleka alikotaka
yeye, akakuhamisha toka katika maisha yako halisi ya sura na mfano wa Mungu
hadi kuwa na sura ya kukataliwa, ukawa ni mtu wa mikosi na balaa za kila aina
hukupata msaada wowote na hakutaka utoke wala hakutaka urudishe maisha yako
tena
Usimuzowee muovu shetani, atakuibia
tena,
Imeandikwa Yohana 10:10 Mwivi huja ili aibe, kuua na
kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele.
11‘‘Mimi ndimi Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema huutoa
uhai Wake Kwa ajili ya kondoo.Usikubali mauti tena katika maisha yako kwa nini
upate shida ikiwa Mchungaji mwema yupo ambaye hawezi kukubali ukavamiwa
ukateswa kama awali,
Jukumu limebaki kwako kama unataka kuwa salama unatakiwa
mar azote uwe makini mawazo yako,akili yako moyo wako mwili wako unatakiwa
kuelekezea kwa Mungu.
Imeandikwa Nahumu 1;9 Unawaza
Nini juu ya BWANA ili akomeshe mateso yako? Hayatainuka
mara ya pili....
Hali ya aina yeyote ikikukuta hutakiwi kurudi kule ulikokuwa
kutafura msaad wewe Imeandikwa Zaburi 50:15 na uniiite siku ya taabu nami
nitakuokoa nawe utanitukuza. Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema: “Una haki
gani kunena sheria zangu au kuchukua agano langu midomoni mwako? Unachukia
mafundisho
Wewe si Kama wao:
Imeandikwa Zaburi 118:17 Sitakufa bali nitaishi, nitatangaza
yale BWANA aliyoyatenda. Wewe si kama wao mateso yao hayatawaacha ila wewe
tayari uko na Ahadi kubwa ya kutokufa japo magumu yamekuandama kwa muda mrefu
sasa yamefika mwisho hakuna jambo lililo na mwanzo likakosa mwisho kila jambo
na wakati wake,
Huu ni wakati wako na haya ni majira yako ya kuishi maisha yako
halisi aliyokusudia Mungu uyaishi hutakiwi kuishi kama zamani tayari marafiki
mazingira matendo yako yanatakiwa sasa yasifanane nayale ya kale,
***************************************************************************
MISINGI MIBOVU SEHEMU YATANO
MAJARIBU: CHANGAMOTO
Mafanikio ya aina yeyote yanaambatana na Changamoto ili kusonga
mbele unahitaji kupambana nazo na uzishende ili ufanikiwe Changamoto ni jiko la
kukupika wewe kufika katika hatima ya maisha yako, usikwepe change mote
usikatae change moto utakosa mahali pakujipimia kama umefikia kiwango gani cha
kumjuwa Mungu,
Kila hatua unayoichukuwa katika hii
Dunia imeambatana na change moto yake kule ulikokuwa mwano kulikuwa na
changamoto zake na sasa huku nako kuna change moto zake ila huku ulipo ushindi
ni mkubwa na wa uhakika maana uko katika ufalme mkuu wa ushindi hauna historia
ya kushindwa,
Ni vema nguvu ya Imani uliyoipokea kutoka kwa Bwana Yesu Ukaanza
kuitumia ili kufika katika mafanikio uliyoahidiwa na Mungu mafanikio yanaenda
kutokea juu ya maisha yako ila si kirahisi kama mtu kuokota maparachichi chini
ya Mti. Haijalishi mazingira uliyonayo hata kama hayaonyeshi ushindi unaoutaka,
lakini unapojaribu kuweka imani juu ya kufanikiwa, amini ndani ya moyo wako ni
rahisi sana kutengeneza mazingira ya kufanikiwa kama ulivyotarajia maana Mungu
si Mtu hata akasema uwongo Hivyo hali Yeyote isikutishe
Imeandikwa Hesabu 23:19 Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si
mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua. Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona
ukaidi katika Israeli. Bwana, Mungu wake, yu pamoja naye,
Maisha ya mwenye haki yanahitaji
Imani
Imeandikwa Waibrania 10:38 Lakini mwenye haki Wangu ataishi kwa
imani. Lakini kama akisita-sita sina furaha naye.” Lakini sisi hatumo miongoni
mwa hao wanaosita na kuangamia, bali tuko miongoni mwa hao wenye imani na hivyo
tunaokolewa Ugumu wa aina yeyote unaokutana nao Usipoteze Imani yako na Mungu
Endelea kumwamini yeye wakati wote mahali popote sehemu yeyete kwa Mtu yeyete,
usikatishwe tamaa na familia au ndugu au mke au mme au watoto wewe songa mbele,
Imani ni jambo muhimu katika kukupa nguvu ya
UVUMILIVU juu ya kila changamoto ngumu unazokutana nazo katika maisha yako.
Hakuna ushindi wowote unaoweza kuupata nje ya kuishi maisha ya imani. Hakuna
mafanikio wala raha ya maisha nje ya kuwa na matarajio makubwa na ushindi
katika maisha yako na kumwamini Mungu imeandikwa
Yeremia 29:11 Mungu anakuwazia yaliyomema tu
kufanikiwa kwa Kila hatua unayohitaji kupiga
kwenye maisha yako kumbuka unahitaji imani ili kuweza kuifikia kama
ulivyotarajia. Kila mara weka imani ili kuweza kujiamini na kuwa na mwelekeo wa
kudumu hata kama utakutana na majaribu au changamoto nyingi njiani.
Usiogope
changamoto unazokutana nazo kikubwa amini zinakuja kwako kwa kuwa wewe ndie
mwenye nafasi kubwa ya kuzitatua. Kumbuka hakuna jaribu lisilo na mlango wa
kutokea na tatizo litakuwa kubwa kulingana na wewe utakavyolitukuza. Tambuwa
kuwa hakuna tatizo linalomshinda Mungu imeandikwa
luka 1:37 Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.” Hao wanaokushambulia
watatulia tu huu ni wakati wao wa
kuongea ila wakati wa kunyamaza unakuja magumu ni njia ya kukupeleka katika
hatua mpya unayotakiwa kufika
Kila
unapoona unapitia kwenye kipindi kigumu kwenye maisha yako amini upo kwenye
wakati wa kupikwa ili kuweza kufanana na nafasi unayoiendea mbele yako. Huwezi
kuwa mtu mkuu kwa kupitia njia rahisi kwa sasa, wala huwezi kuwa mtu wa heshima
bila kuandaliwa katika hiyo heshima ili uwe mkuu ni lazima maisha yako
yatapitia kwenye kila aina ya changamoto zinazokuja kukutengeneza ili ufananie
na nafasi unayoifaata mbele yako.
Ndio
maana unapoona changamoto zinazidi kwako si wakati wa kulia na kukata tamaa
bali ni wakati wa kuishi kwa imani ili kuweza kuzishinda changamoto hizo na
kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Utukufu wa Mungu unaongezeka
kutokana na ushindi wako wa changamoto Unazopitia wewe huhitaji kusikiliza
masikio yako ya inje sana sikiliza masikio yako ya Ndani Zaidi na kile
kilichoyabadilisha maisha yako ni Imani hivyo usiipoteza kirahisi.
Imani
ni kila kitu na inaweza kukupa kila aina ya mazuri unayoyahitaji katika maisha
yako. Hauhitaji kuwa na kila kitu ili uwe na kitu, bali unahitaji kuwa na imani
ili uwe na kila kitu unachotarajia. Ndio maana chochote unachokihitaji katika
maisha yako hata kama kina ukubwa wa aina gani kama ukianza kwa kuamini
umekipata na kuchukua hatua kukitafuta kwa vitendo uwe na uhakika utakipata
mikononi mwako. Hiyo ndio imani, ni kuwa na uhakika wa kweli ndani yako ‘’moyoni
mwako’’wa kile kitu unachotarajia.
Uhakika wa ushindi katika majaribu au
magumu unayopitia
Imeandikwa Waibrania 11:1
Imani ni kuwa na uhakika wa mambo mazuri unayoyatarajia katika maisha
yako. Imani ni kujenga picha ya maisha yako ya badae unavyotaka yawe ukiwa
unaishi sasa. Leo amua kuishi kwa imani zaidi juu ya kesho Zaidi ya jana kile
unachotarajia kwenye maisha yako ikiwemo kufanikisha ndoto ya hatima ya maisha
yako uliyonayo. Hakika utauona ushindi mkuu ukitokea dhidi yako. Kila mara
jiulize, Je, ninatembea na kuishi kwa imani juu ya kile ninachotaka?
Maana
pasipo Imani imeandikwa sitampendeza Mungu Je kwa Imani niliyokuwa nayo
Ninampendeza Mungu? Hakuna jaribu kubwa kwa Mungu yote yanakuwa makubwa
tunapoyakuza katika akili zetu za darasani amini ishi kwa Imani shika Imani
tendea kazi Imani utaona matokeo ya Imani Mungu anaitazama Imani yako
kukutendea anangoja kuona ushindi juu ya jaribu ugumu unaopitia, ukiisha amina,
Somo; Maisha ya Ushindi
Warumi
10:38 warumi 10:10 waefeso 6:12
Utangulizi:
Lolote
unalolihitaji katika hayamaisha nilazima ulifanyie kazi na inawezekana na
wengine wanalitaka pia hivyo maisha ni ushindani, wanaokwenda vitani pande zote
wanategemea ushindi, wafanyabiashara wanategemea faida,wanafunzi wanandoto
zakuja kuwa watu wenyenafasi kubwa katika jamii
kila mtu anapenda kuwa tajiri lakini si kila mtu ni tajiri kila mtu
anapenda kuokoka lakini sikila mtu ameokoka wakristo ni wengi wenye Imani ni
wachache, jambo lolote unalotaka kufanikiwa linahitaji ujuzi wa kulifanya,
Ushindi wa kiroho ni upi?
Ushindi
wa kiroho ni ushindi unaopatikania katika ulimwengu usioonekana kwa macho ya
kawaida bali ushindi huo unaanzia rohoni na kukamilikia mwilini yaani macho ya
kiroho yanaanza kasha ya mwili
Ili
mtu aitwe mshindi lazima kunapambano amepambana akaushindi ugumu uliokuwa
kipingamizi au maadui zake sasa anaitwa mshindi, hapa tunajifunza namna ya kuwa
mshindi wa kiroho maana ndiko kila jambo linakoanzia, hii ndiyo sababukubwa ya
maisha yakiroho yanahitaji Imani imeandikwa waibrania 10:38 Lakini mwenye haki
Wangu ataishi kwa imani.
o Lakini kama akisita-sita sina furaha
naye.”
o Maisha ya mwenye haki ni ya Imani
o Uhalali wa wewe kuponywa magonywa
yote ni kuwa na imani
o Haki ya kurejeshewa yote yaliyopotea
o Haki ya kurejeshewa ndoa na afya,
o Haki ya kurithi mafanikio yako yote
inahitajika Imani
o Kuhudumiwa kwa namna yeyote
unayohitaji unahitaji kuongeza Imani yako,
Maisha yetu halisi tunayotakiwa
kuishi ni Imani Mungu ameturudishia kwanjia ya Imani, imeandikwa Warumi 10:10 Kwa maana Kwa moyo mtu huamini na hivyo
kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu. Kama
yasemavyo Maandiko, ‘‘ye yote amwaminiye hatatahayarika.’
Hakuna namna yeyote unayoweza kuhesabiwa haki au kupata uhalali
wa maombi yako bila Imani. Maombi yeyote yake yanahitaji Imani, kushinda
vikwazo kushinda majaribu kupita katika kila ugumu unatakiwa kuamini kwamba
unaweza,
Imeandikwa waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu si juu ya
nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi
ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu
ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote,
simameni imara. Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa
dirii ya haki kifuani, 1nayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya
amani. Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani,
Ambayo kwa
Hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu.
Mkiomba Kwa Roho sikuzote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati
mkiwaombea watakatifu wote kupambana kwetu si juu ya Damu na nyama
Imeandikwa waibrani 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo
yatarajiwayo, ni udhahiri wa mambo yasiyoonekana. Naam, Kwa imani baba zetu wa
kale walishuhudiwa.
Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa Kwa neno la
Mungu, vitu vyote vinavyoonekana viliumbwa Kwa vitu visivyoonekana.
Maisha ya ushindi yanatokana na Upande
wenye nguvu
v
Maisha ya ushindi yanapatikania ndani ya ufalme wa kiroho na si
wa kimwili na hiyo ndiyo sababu macho ya
kawaida hayawezi kuona,
v
Maisha ya ushindi yanaambatana na Mamlaka za Kiroho
v
Maisha ya kiroho lazima uwe umejikamilisha kwa kuvaa sila zote
za kiroho
v
Maisha ya ushindi unatakiwa kusimama imara wakati wote,
SLaha za kiroho juu ya ushindi wako
Mtu wa Mungu lazima awe mkeli asiwe na lugha mbili
Mtu wa Mungu lazima awe ni mtu wa mhaki fuani, 1nayo miguu yenu
ifungiwe utayari
Mtu wa Mungu alima awe na Utayari
Mtu wa Mungu lazima awe na Imani kuu isiyo na mashaka
Ulimwengu wakiroho ushindi unaupata kutoka kwa Mungu imeandikwa Isaya 66:2 Je, mkono wangu
haukufanya vitu hivi vyote, hivyo vikapata kuwepo?” asema BWANA. “Mtu huyu
ndiye ninayemthamini: Yeye ambaye ni mnyenyekevu na mwenye roho yenye toba,
wewe ni mshindi kwakuwa macho ya Mungu yanakutazama wewe, wakati wote juu ya
kile unachokifanya na mahali popote ulipo,
Umechaguwa njia njema Sana na upande wenye nguvu kubwa kuliko
kote,
Imeandikwa Yeremia 1:12BWANA akaniambia, “Umeona vyema kwa maana
ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba nimelitimiza.’’
Hapatakuwa na Adui wa Kukushinda wewe
Imeandikwa Yeremia 30:16“‘Lakini watu wote wakuangamizao
wataangamizwa, adui zako wote watakwenda
Uhamishoni. Wale wote wakutekao nyara
watatekwa nyara,
Wote wakufanyao mateka nitawafanya
mateka. Lakini nitakurudishia afya yako na kuyaponya majeraha yako,’asema
BWANA,
Muongozo wa ushindi wa kudumu ishi maisha ya maelekezo
Imeandikwa Yoshua 1; Usiache Kitabu hiki cha Torati
kiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, ili upate
kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake.
Ndipo utakapoifanikisha njia yako na kisha utasitawi sana. Je, si Mimi
niliyekuamuru? Uwe imara na hodari sana. Usiogope wala usivunjike moyo, kwa
kuwa BWANA wako, atakuwa pamoja nawe ko kote uendako.’
Usiogope maana ufalme uliyopo
unanguvu sana kuliko kule ulikokuwa
Imeandikwa Isaya 41:10 Hivyo usiogope, kwa maana niko
pamoja nawe,
Usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu
wako. Nitakutia nguvu na kukusaidia,
Nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa
haki yangu. 11“Wote walioona hasira dhidi yako hakika wataaibika na
kutahayarika, wale wakupingao watakuwa kama vile si kitu na kuangamia. Ingawa
utawatafuta adui zako,
Hutawaona. Wale wanaopigana vita
dhidi yako watakuwa Kama vile si kitu kabisa. Kwa maana Mimi ndimi BWANA, Mungu
wako,
Isaya 65:24 Kabla hawajaita nitajibu, nao wakiwa katika
kunena nitasikia kumbe ufalme wa Mungu hata kabla hujamwambia Mungu amesha
juwa………………………….