Jibu la maswali yako ni Neno la Mungu
1: Biblia ni neno timilifu la Mungu, linalo
ongoza kwa Roho Mtakatifu, na lina kila jibu la matatizo ya mwanadamu. (2
Timotheo 3:16-17 na 2 Petro 1:20-21).
2: Kuna Mungu mmoja , aliye katika namna
tatu : Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. (Yohana 10:30 , Yohana
14:26 na Wafilipi 2:5-7).
3: Mungu ni pendo na anapenda watu wote. Ni
shauku yake kufikia watu ambao ni maskini , waliodhulumiwa,walio wajane au
yatima, na kuponya waliovunjika mioyo .(Zaburi 68:5 - 6 na 1 Yohana 4:16).
4: Mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu
lakini dhambi imemtenga na Mungu. Bila Yesu hatuwezi kuwa na uhusiano na
Mungu.(Mwanzo 1:26 na 1 Timotheo 2:05).
5: Tunaweza kuwa na uhusiano binafsi na
Mungu kwa njia ya wokovu, karama ya bure ya Mungu kwa mwanadamu. Sio matokeo ya
ambacho tunakifanya, ila tu inapatikana kwa msaada wa bure wa Mungu. Kwa kukiri
tumetenda dhambi na kuamini katika kufa, kuzikwa, na kufufuka kwa Kristo , na
kumkubali Yeye kama Bwana , tunaweza kuwa na Mungu milele. (Waefeso 2:8 - 9 ;
Warumi 5:1 na Warumi 3:24)
6: Tunaamini katika ubatizo wa maji , kama
ilivyofundishwa na kuoneshwa na Yesu, kama njia kwa ajili ya waaminio kutambua
kwa kufa, kuzikwa, na kufufuka kwa Yesu. (Mathayo 28:19; Warumi 6:04 and
Mathayo 3:13-17).
7: Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni zawadi kutoka
kwa Mungu. Husaidia kumwezesha muumini kuendeleza tabia ya Kristo na kuishi
kila siku katika mapenzi ya Mungu. (Mathayo 3:11 and Matendo 2:04).
8: Mungu huwapa wote waaminio karama za
kiroho. Wao ni kwa ajili ya kuimarisha watu wa Mungu ( Kanisa) na kuthibitisha
uwepo na nguvu za Mungu kwa wasioamini. Zawadi ya Roho ni hai na ni muhimu
inayohusika leo . ( 1 Petro 41 Wakorintho 12:4-11 and:10).
9: Utakaso ni mchakato unaoendelea wa
kuruhusu tabia ya Mungu kukuwa ndani yetu. (Warumi 6:19 na Wagalatia 5:22-25).
10: Uponyaji wa Mungu ni hai katika maisha
ya leo kupitia Yesu Kristo, ambaye ni Mponyaji. Uponyaji ni pamoja na kimwili,
kiakili, kihisia na mrejesho wa kiroho. (Luka 9:11; Mathayo 9:35; Matendo 10:38
na Mathayo 10:1).
11: Biblia inaeleza kuzimu kama mahali
halisi. Ni mahali pa mateso na mahali pa kujitenga kabisa na Mungu kwa wale
wanao kufa bila ya kumkubali Kristo. Shahuku ya Mungu ni kwamba hakuna
atakayetengwa na yeye milele , ndiyo maana alimtuma Mwana wake , Yesu Kristo,
duniani. (Waebrania 9:27 , Ufunuo 20:12-15 na Yohana 3:16-18).
12: Yesu atarudi na kuchukua waliompokea
kama Mwokozi kuwa pamoja naye milele. (Matendo 1:11 , 1 Wathesalonike 4:13-17
na Waebrania 9:28).