Powered By Blogger

Wednesday, 14 March 2018

MUNGU KWANZA- MATHAYO 6:33




 UTANGULIZI:
Namna unavyojifunza unaongeza nguvu ya kufanikiwa katika maisha yako kwakuongeza ufahamu,

Jiulize huwa unapokea taarifa na maelekezo kutoka kwa nani? Huwa unamsikiliza nani zaidi kila mara, anayekuhamasisha na kukusogeza kwenye hatima njema ya maisha yako na ndoto uliyonayo? Kumbuka utakuwa vile utakavyokuwa kesho kulingana na mtu unayetoa nafasi kubwa zaidi ya kumsikia mara kwa mara na kila siku.
Ni vyema leo uamue kuwasikiliza watu wachache wenye kuweza kukufanya uwe na matokeo makubwa katika maisha yako.

 Sikiliza watu wenye kuleta matokeo, watu wenye “impact” kwenye hii dunia na jamii yao, watu waliojaa “action” na sio hadithi za kale (za kizee), watu waliotambua makusudi makubwa ya maisha yao na kuamua kuyafanikisha kwa dhati na kwa kujitoa kwa kila namna. Huwezi kuwa mbadala wa yule unayempa muda kila siku kumsilikiliza na kumfatilia mara kwa mara.

Maisha yetu kiujumla yanathiriwa sana na wale watu tunaowapa muda kuwasikia na kusoma juu ya vitu vyao wanavyoviandika. Leo amua kuwa na mtu chanya katika mwenendo wako, mtu mwenye matokeo ya wazi yanayoonekana, mtu unayeweza kumfatilia mara kwa mara ili akupe msukumo wa ndani kwenye lile unalofanya linalofanana na analofanya yeye ili aweze kukusaidia kulifanya kwa ubora zaidi ya hapo ulipo sasa. Ni muhimu kuwa na watu sahihi na kwa majira sahihi ili wakujenge kwenye kile unachotaka kufanikisha.

“The distance between you and your next level is an instruction” -Emmanuel Makandiwa
Nataka ujiulize leo kwa mara nyingine tena, ni mhubiri gani huwa unamsikiliza? Ni mwimbaji gani huwa unatoa muda mwingi kusikiliza nyimbo zake? Ni vitabu vya aina gani na vya mtu gani huwa unasoma zaidi? Ni mtu gani huwa unakaa naye muda mrefu kufanya mazungumzo nae, na Je, huwa mnaongea nini mkiwa pamoja? Ni mtu gani unayesoma post zake zaidi kwenye mitandao ya kijamii? Hao wote wanayo nafasi ya kubwa ya kukufanya wewe uwe vile utakavyokuwa kwenye maisha yako ya badae. 

Wote wana mchango wa kukujenga au kuharibu kabisa maisha yako ya sasa na ya badae. (Remember that, your instructor determine your future).
Leo amua kuchagua mtu sahihi wa kumsikia au kumsikiliza au kusoma post zake mara kwa mara kila unapopata nafasi ya kufanya hivyo. Kumbuka nimekuambia mtu unayemsikiliza mara kwa mara ndiye atakayekufanya uwe kwenye viwango gani vya maisha hapo badae, amua leo kuchagua mtu sahihi ili ufikie viwango sahihi ambavyo Mungu amekutazamia

MAONO
Maono ni hali halisi ya kuona kesho yako njema (future) ukiwa unaishi sasa. Maono ni kuona kwa picha unachokitarajia kwa muda mrefu tena pasipo kuchoka. Maono ni picha halisi iliyomo moyoni mwako inayokupa mwanga wa kule unakoelekea. Maono ni daraja kati ya leo yako na kesho yako, maono yanakuunganisha na kesho yako ukiwa unaishi leo, bila maono utapotelea mahali usikojua, au utaenda mahali usikotaka.

Kila mmoja anataka kufanikiwa juu ya eneo fulani katika maisha yake. Moja ya mambo ambayo ni muhimu sana kujua au kuwa nayo ili kufanikiwa ni kuwa na picha ndani yako, picha ya kile unachokitaka, picha ya kule unakotaka kwenda. Picha hii ni muhimu sana, picha hii ina uzito wa kipekee usioelezeka kwa ajili ya wewe kufikia kule unakotaka, au kupata kile unachokitaka.

Picha hii ninayoizungumzia hapa huitwa au kutajwa kama maono kwenye maandiko na sehemu nyinginezo. Ni nyenzo muhimu sana kwa ajili ya safari ya mtu ambaye ana nia ya kweli ya kufanikiwa. Ili mtu aweze kufanikiwa kwenye eneo lolote lile analotarajia mafanikio ni lazima awe na maono, awe na picha hiyo ndani yake siku zote kabla ya kuifikia.
Kama mtu anataka kujenga, kumiliki gari, kuwa na biashara kubwa nk, ni lazima ajifunze kwanza kuwa na nyumba hiyo ndani yake, awe na hiyo gari au hiyo biashara kwenye nafsi yake. Ni muhimu sana aweze kuona anachokitarajia kwenye macho yake ya ndani hata kama wengine watashindwa kukiona anachokiona kwa sasa, MAONO!

Ukweli halisi ni huu kuhusu Maono:
1: Huwezi kuwa na maono ukakosa tumaini; na huwezi kuwa na maono ukakosa imani. Na huwezi kuwa na maono ukakosa uaminifu. Mtu mwenye maono anayo imani ya kuamini ipo siku atafikia anachokiona ndani yake hata kama mazingira ya sasa hayaoneshi hali halisi ya kufanikiwa kwake.

2: Maono yanaweza kukufanya usife mapema. Mungu anaweza kusitisha hatua ya kuchukua uhai wako kulingana na ukubwa wa maono uliyonayo hasa kama yanagusa maisha ya watu wengine zaidi.
Maono ni njia mojawapo ya kuongeza nafasi ya kuishi, Mungu anathamini wanaoona zaidi kuliko wanaoangalia. No vision No life.
Hata kama kuna watu wamepanga mabaya ya kutisha juu yako (kukuua au kukudhuru) ni ngumu kufanikiwa kama umebeba maono makubwa ndani yako. Maono yana tabia ya kulinda uhai wa mtu dhidi ya watesi na wabaya wake.

3: Huwezi kuwa na maono makubwa ndani yako ukaruhusu urafiki au ukaribu na kila mtu. Maono ndio yanayokuchagulia marafiki na watu wa kuishi nao kwa karibu.
Mungu akikupa maono ndani yako uwe na uhakika ni lazima akupe na watu wa kwenda nao, huwezi kuwa na maono ukaruhusu mazoea na kila mtu.

4: Kijana; Maono ndio yanayokuchagulia mke au mume wa kuwa nae maishani, na si kwa vigezo vya nje unavyoviangalia kwa Sasa. Unaweza kuchagua mke au mume mwenye sura na muonekano mzuri wa kifedha au elimu; lakini akikosa maono ndoa imekosa msimamo na mwelekeo.
Ndoa, kampuni au mtu binafsi akikosa maono amekosa Msimamo. Ukikosa msimamo umekosa mwelekeo (focus). Ukikosa mwelekeo ni rahisi sana kuishi maisha ya kubahatisha.
“Maono ni njia mojawapo ya kuongeza nafasi ya kuishi, Mungu anathamini wanaoona zaidi kuliko wanaoangalia.”
-Wilfred Tarimo
5: Huwezi kuwa na maono ya muda mrefu ukaruhusu kula au kunywa kila kitu. Mtu mwenye maono hawezi kula au kunywa kila kitu kinacholetwa mbele yake.
Maono yana tabia ya kulinda afya. Ukiwa na maono ya muda mrefu si rahisi kula kila chakula au kinywaji kinachopita mbele yako.

6: Kijana; Maono ndio yanayokuchagulia Course gani ya kusoma shuleni/chuoni na si soko la ajira mtaani. Huwezi kuchagua kusoma chochote kisichoendana na matazamio ya maono yako uliyobeba moyoni.
Huwezi kuwa na maono fulani ukaruhusu ubongo wako kusoma kila kitu.

7: Maono ndio yanayokupa mfumo wa maisha (life style) itakayokufanya uwe tofauti na watu wengine hata wao kutamani kuishi au kuwa kama wewe.
Huwezi kuwa na maono ukaishi maisha ya kuigaiga, mtu mwenye maono hana ku_copy na ku_paste kutoka kwa wengine.

8: Maono ndio yanayozaa nidhamu (discipline) juu ya kufanya maamuzi mbalimbali ikiwemo maamuzi juu ya matumizi ya fedha zako, au kuchagua marafiki wa kwenda nao, au chakula au vinywaji gani vya kutumia.

9: Huna maono, Huna maisha. Ni rahisi kuzaa hasara na kufa pasipo faida baada ya kuishi pasipo maono.
Je, unaona nini? Unajiona wapi miaka 5 au 10 au 20 ijayo? ongeza ufahamu kwakujifunza zaidi, Mungu kwanza mathayo 6:33

Ninawezaje Pata amani?

Unawezaje kupata amani? Baba Nabii akifunua siri ya kuwa na amani kama ya kwake aliyonayo Utangulizi kazi kubwa kabisa kwa Mwanadamu...