Unapotendewa ubaya na Adui ufanye Nini
Utangulizi:
mara nyingi watu wanapenda vitu vizuri watendewe na wengine ila wao wenyewe hawako tayari kuwatenendea mazuri wengine .kabla hujasema kwanini mimi jiulize na wewe umefanya nini kwa mwingine?
Tunapaswa kuwa tendea vipi maadui wetu? imeandikwa Luka 6:27-36 "Lakini
nawaambia ninyi mnaosikia wapendeni adui zenu watendeeni mema wele ambao
wawachukia ninyi wabarikieni wale ambao wawalani ninyi waombeeni wale
ambao waonea ninyi akupigae shavu moja mgeuzie lapili naye
akunyang'anyaye joho lako usimzuilie na kanzu mpe kila akuombaye na
akunyag'anyaye vitu vyako,
usitake akurudishie nakama mnavyo taka watu
wawatendee ninyi watendeeni vivyo hivyo
Maana mkiwapenda wele wawapendao ninyi mwaonyesha fadhili gani? kwa kuwa
hata wenye dhambi wawapenda wale wawapendao nanyi mkiwatendea mema wale
wawatendeao mema mwaonyesha fadhili gani? hata wenye dhambi hufanya
vivyo hivyo. Na mkiwakopesha watu vitu huku mkitumaini kupata kitu kwao
mwaonyesha fadhili gani? hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi ili
warudishiwe vile vile basi wapendeni adui zenu tendeni mema na kukopesha
msitumaini kupata malipo na dhawabu yenu itakuwa nyingi nanyi mtakuwa
wana wa aliye juu kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasio mshukuru na weovu
basi iweni na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma."
Tuwatendee maadui zetu kwa roho njema. Imeadikwa Mathayo 5:25 "Patana na
mshitaki wako upesi wakati uwapo pamoja naye njiani yule mshitaki asije
akakupeleka kwa kadhi na kadhi akakupeleka kwa askari ukatupwa
gerzani."
Usifurahi katika majonzi ya adui zako. Imeandikwa Medhali 24:17-18
"Usifurahi adui yako aangukapo; wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;
Bwana asije akaliona hilo likamkasirisha akgeuzia mbali naye hasira
yake."
Imeandikwa Warumi 12:20 "Lakini adui yako akiwa na njaa mlishe akiwa na
kiu mnyeweshe maana ufanyapo hivyo utampalia makaa ya moto kichwani
pake."
Mungu ametuahidi kutuhifadhi kutokana na maanui wetu imeandikwa Zaburi
18:48 "Hutniponya na adui zangu naam waniinua juu yao walioniinukia na
kuniponya na mtu wa jeuri."