EPUKA WEZI WA MAWAZO
Utangulizi:
Kihualisia Mungu ametoa upendeleo kwa kila mwanadamu awe na kichwa chake japo kuna watu wanatumia vichwa vyao na bado wanataka watumie na vichwa vya watu wengine, Mungu amefanya hivyo ili kila mmoja aweze kuwaza na kuamua juu ya maisha anayoyataka,
Sasa kuna watu ambao mimi nawapa jina la wezi wa mawazo ya watu, wao wanataka kile wanachokiwaza kionekane ni saghihi hatakama si sahihi ilimradi wao wanaona vile wanavyo ona basi wanalazimisha wengine waone hivyo ikiwezekana hata katika vitendo wafanye kama wanavyotaka au kupenda wao hilo naliita wizi wa mawazo iwe kwa ushawishi au kwa kupewa zawadi huo ni wizi wa mawazo,
Katika maisha Mungu amekuwekea muelekeo wako kwaajili ya kufanikiwa soma bibilia yako wana waizraeli walipitishwa katikati ya bahari si kwamba walipenda ila ilitakiwa wapite hapo kwaajili ya kufika kule walikotakiwa kwenda,
Tatizo lolote linalokuandama usilikimbize kwa watu mpelekee Mungu Huruma za watu ni za muda mfupi sana leo ukipata tatizo watakuja na watakuonyesha machozi kama wako pamoja na wewe siku tatu tu wamesahau maumivu unabaki nayo wewe kama wewe,
wakati mwingine wanakuliwaza kumbe ndiyo hao hao wanaosababisha maumivu yako imeandikwa mathayo 10:36 na Adui za Mtu ni wale wa nyumbani kwake, si kila mtu anayekuonyesha anakupenda ni kweli yuko upande wako.
Tumia akili yako kuishi maisha unayoyapenda tumia akili yako jifunze kwa watu maamuzi na vitendo jitahidi viwe vya kwako usiishi kwakupangiwa maisha unayotakiwa kuishi wewe kama wewe,
kuwa makini,jiepushe na wezi wa mawazo,hao wanapatikana kila mahali,katika mabasi,masokoni,katika majumba ya ibada,katika mitandao, wanachezea akili yako usikubali kufuata kitu usichokitaka katika maisha yako, kila unalolifanya jiulize mara tano linafaida kwa nani,linafaida kwalini,kwanini ufanye .