Powered By Blogger

Wednesday, 14 March 2018

USITAFUTE MAFANIKIO YAKO KWA MTU MWINGINE YAKO KWAKO



Nguvu na Msukumo wa Kuchukuwa Hatua ya mafanikio
UTANGULIZI:
kuna mambo machache unaweza kujifunza hapa na kukajikuta unapata mafanikio makubwa sana

mfano :
Ukipanda mbegu moja ya maindi ikiota na ikazaa muhindi utakuwa umevuna mbegu zaidi ya 10,000 kwa muindi mmoja hivyo tafuta ufahamu kwa gharama yanamna yeyote, usitafute mtu wa kumlahumu, haitakusaidia zaidi ya kukuumiza,

mafanikio unayoyataka hayako kwa mtu yako kwako,

Maisha si marahisi wakati wote kama wengi wanavyozani hasa pale unapokutana na changamoto mbali mbali zinazoweza kuwa kizuizi kikubwa juu ya jambo lako zuri unalotaka kulitimiza kwa wakati fulani.

Kuna wakati unaweza ukawa unatamani kukamilisha wajibu fulani mkubwa mbele yako, ili uweze kufikia hatua ya juu ya kufanikiwa na kuleta matokeo chanya katika maisha yako lakini hali ikawa tofauti na unavyotaka iwe kwa kipindi hicho. 

Yawezekana unahitaji kuchukua hatua kwa ajili ya kukamilisha malengo na mipango yako mizuri uliyonayo lakini kila unapootaka kufanya hivyo unakosa msukumo na nguvu ya kuchukua hatua husika.

Ninawezaje Pata amani?

Unawezaje kupata amani? Baba Nabii akifunua siri ya kuwa na amani kama ya kwake aliyonayo Utangulizi kazi kubwa kabisa kwa Mwanadamu...