Anza na hatua ndogo kwanza. kubwa itafuata usiogope watu
Mtu wa Mungu Kulia akihamasishana na Mkewe juu ya safari ya maisha,
Wapo watu wengi kila wanapotaka kutimiza malengo yao na mipango fulani waliyonayo huwa ni watu wa kusubiri wafanikishe kwanza hatua fulani kubwa itakayoweza kuwaletea mafanikio ya haraka kabla hawajapita kwenye hatua ndogo zinazoweza kuwa msingi mzuri wa kule wanapoelekea. Anza kidogo kidogo kwa ulichonacho;
anza kuchukua hatua ndogo leo hii ili uweze kuleta matokeo madogo yanayoweza kuzaa njia mpya na pana ya kukupeleka katika mafanikio mengine makubwa zaidi.