Na Baba Nabii Samson Mboya
MAISHA YA USHINDI -IMANI
Utangulizi:ili kuishi Maisha ya
ushindi unahitaji kuwa na imani kuu juu ya ushindi uliyopata kutoka Ka Mungu,
uliyemwamini,
Imeandikwa waebrania 10:38
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina
furaha naye.
Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.
Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.
Kumbe haki ya mwana wa Mungu
inapatikana kwanjia ya imani
v Mwenye haki wa Mungu ataishi
kwa kumwamini Mungu
v Akisali anamwamini Mungu ameshajibu Maombi yake Imeandikwa
Isaya 65:24 kabla ya kuoamba nitajibu ukiwa katika kunena nitasikia,
v Lazima fikira zako uziamini juu ya kile unachokiwaza
v Lazima maamuzi yako uyaamini bila mashaka
v Lazima msimamo wako uuamini kuwa hukukosea kumwamini Yesu
v Lazima ujiamini hata wewe mwenyewe kwamba uko katika njia
sahihi ya Mungu mwenyewe
v Lazima uamini ulipomwamini Yesu kristo kuwa bwana kuwa bana
na muokozi wa maisha yako uliingia katika ufalme mpya
v Lazima uamini uhamisho wako ulifanyika kweli na uamini
maisha mapya ya ufalme wa nuru imeandikwako wakolosai 1:13 nayealituhamisha
kutoka katika ufalme wa giza,
v Kuwa na mashaka juu ya imani yako kwa Mungu ni chukizo kwa
Mungu,
v Lazima uamini kwa tangu ulipomwamini Yesu wewe ulihamishwa
kwenye wasiwasi,mashaka huzuni,mateso magonjwa maisha machafu ni mwiko kwako
sasa,
v Maisha ya imani yanafaida kwa na ushindi usiyowa kawaida,
maana hakuna cha kukutisha kwa namna yeyote,
Imani nini? Imeandikwa waebrania 11:1 "Basi imani ni kuwa na hakika ya
mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana." Imani nikuwa na
uwakika ya juu ya kile kitu unachokitarajia kuwa nacho au kikipata katika
maisha yako ambacho kwa wakati huo hakipo mikononi bali unakitarajia kukiona na
kukichukuwa,
Yesu ndiye mwanzo wa imani imeandikwa Luka 17:5 "Mitume
wakamwambia Bwana tuongezee imani."Imeandikwa
Warumi 10:17 yasema "Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia
huja kwa neno la kristo."
Imani ya haki ni kuamini yote ambayo
Yesu ametutendea. imeandikwa Warumi 5:1 "Basi tukiisha kuhesabiwa haki
itokayo katika imani, na mwe na imani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu
kristo."
Imani ni kuwa na hakika juu ya ahadi
zote za Mungu alizoziahidi Imani ni kuwana imani kwa Mungu katika mambo yote.
imeandikwa Waebrania 10:38 "Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani
naye akisita-sita Roho yangu haina furaha naye."
Imani dhaifu yaweza kuwa yenye nguvu
Mungu akimsaidia mtu imeandikwa Marko 9:24 "Mara babaye yule kijana
akapaza sauti akasema Naamini nisaidie kutokuamini kwangu." Kumbe unaweza kusaidiwa na Mungu katika
kutokuamini kwako,