Powered By Blogger

Wednesday, 14 March 2018

Mnara wa mateso

Imeandikwa mwanzo 11:1-9
Watu wakajenga mnara kwenda mbinguni,kama walimjengea Mungu mnara je, watu haohao watashindwa kukujengea na wewe? Kuna watu wanaishi katika mateso maana wamejengewa minara ya madeni, magonjwa,shida ,mikosi ,balaa na shida mbalimbali, .Kumbe Kuna mnara unaowatesa  .
Imeandikwa mwanzo 1:26
Mungu akasema na tumfanye mtu kwa sura yetu namfono wetu akaijaze nchi .lakini watu wakamuasi Mungu kwa kutofuata maelekezo,  wakajikusanya na kujijengea mnara ili kujijengea heshima ya majina yao.
Unapoteseka adui yako anafurahia sana.wanakaa vikao na kushauriana ,wakujengee mnara wa aina gani, mnara wa magonjwa,kukataliwa, madeni, au kuvunja ndoa. Vikao vyao wanajua wanapovifanyia,Ni vikao vyao kiroho huwezi kuviona  kwa macho ya kawaida .Na huwa Wana maeneo maalumu ya kufanyia vikao hivyo.
Ili uweze kuwashinda na kuwachafulia lugha unahitaji msaada wa Mungu kupitia maombi ya kuchafua lugha zao na kubomoa hiyo minara.

Ninawezaje Pata amani?

Unawezaje kupata amani? Baba Nabii akifunua siri ya kuwa na amani kama ya kwake aliyonayo Utangulizi kazi kubwa kabisa kwa Mwanadamu...