USILALAMIKE UMEZUILIWA ,UMEJIZUWIA WEWE MWENYEWE
Malalamiko ya watu wengi unapoyasikiliza wanatupa lawama kwa wengine ila wao hawatafuti wamechangia asilimia ngapi kuharibu maisha yao kwa tabia zao wenyewe,kwa kuiga wengine,kwa kufuata mkubo, kwa kutojitambua,
hakuna tatizo la wengi tatizo ni vile mtu analiona,maana hata kama ni kifo si kila mtu anaogopa kifo, wakati watu wanapanga foleni osipitalini kwaajili ya matibabu wengine wanajinyonga,wanakunywa, sumu,
Mambo mengi umeghairisha kwa sababu ya kukosa msukumo binafsi wa kuchukua hatua za kivitendo na hatimaye umeshindwa kuleta matokeo chanya katika maisha yako.
Wapo watu wengi kila wanapojaribu kupanga jambo fulani wanapanga vizuri, ila unapofika wakati wa kutaka kuchukua hatua wanakuwa wanakosa msukumo na nguvu ya ndani ya kuwasaidia kutimiza wajibu walionao ili kuleta matokeo na mabadiliko makubwa katika maisha yao. Je, na wewe ni miongoni mwa watu wa namna hii?
Soma makala hii ili kuchukua hatua ya mabadiliko yako leo hii.