KUHARIBU MADHABAHU YA ADUI JUU
YA MAISHA YAKO
Na Mtu wa Mungu
Nabii Samson
Somo: KUHARIBU MADHABAHU YA ADUI
JUU YA MAISHA YAKO
Utangulizi
Kimsingi kufanikiwa au kuharibikiwa lazima ufahamu kuwa ipo
madhabahu inayowezesha maisha ya mwanadamu na utaona Muongozo wa Neno la Msingi
linaanza na kusema Mungu ametuweka ili kung’oa kubomoa, kuharibu kuteketeza,
kuangamiza na kupanda na kujenga, huwezi kubomoa kitu ambacho hakija jengwa,
wala huwezi kungoa kitu ambacho hakijaoteshwa pitia maandiko haya kabla
hujaendelea,
Neno la Msingi na vipengele vyake Saba, Yeremia 1:10,Hosea
4:6, Zaburi 18: 1-50, Waamuzi 6:1-40,
1. MADHABAHU NI NINI
2. KAZI YA MADHABAHU
3. AINA ZA MADHABAHU
4. UHARIBIFU WA MADHABAHU
5. MADHABAHU HUWA INAONGEA-INAAGIZA
6. MIFANO YA WATU WALIYO WAHI KUJENGA MADHABAHU
7. MAMLAKA TULIYO PEWA NA MUNGU
8. BAADA YA KUIHARIBU MADHABAHI,
9. HITIMISHO
Madhabahu ni
nini?
Madhabahu ni Eneo lililo tengwa kwa kazi maalumu lakini pia silazima liwe eneo hata kitu
kinaweza kuwa kama madhabahu kwamfano mti maarufu wa aina flula au jiwe,mto,bwawa
na vingine vingi, hiyo ni mifano mochache tu,
Kazi ya madahabahu:
Kazi ya Madhabahu ni kupokea malalamiko kujibu malalamiko ya
watu au mashitaka ya watu wanayoitumiakia ile madhabahu kulingana na maagano ya
Madhababu hiyo,
- 3. AINA ZA MADHABAHU
- Madhabahu yaki-Mungu
- Madhabahu ya shetani
Madhabahu ya shetani ni moja ila maagano ya madhabahu hiyo
ni tofauti sasa hayo maagano ndiyo yanasababisha mtu kujenga kulingana na
mazingira na utamaduni, kwa mfano kila kabila lina mila na utamaduni wao, na
katika upande wa Miungu ni ile ile maana baba wa mizimu (Mizimu) ni Shetani
Uharibifu wa Madhabahu
Madhabahu ya Shetani inaleta uharibifu inatenda kazi sawa
sawa na maagizo ya watu waliokwenda kupeleka malalamiko yao, kwahiyo Madhabahu
inasimamia yale yaliyopelekwa madhabahuni sasa ina tengemea Madhabahu
inayofanya kazi kwako ni ya namna gani ikiwa ni ya shetani basi
yatakayotekelezwa ni ya huyo kuhani,ila ikiwa ni ya Mungu utapata uzima na
mema, kwa usalama wako lazima ukubali huharibu madhabahu moja ili itumike maja
huwezi ukahudumiwa na madhabahu mbili,
Kipindi ambacho Taifa la Israel walipokuwa watumwa wa
wamidian, watu walikuwa wanaonewa sana na kunyang’anywa mali zao hata mazao yao
yalikuwa yakiharibiwa. Hivyo Gidion alikuwa amejificha kwenye mwamba akipepeta
ngano ndipo malaika akamwita ewe shujaa Gidion,, lakini Gidion alikataa kuitwa
shujaa kwa maaana alikuwa hajiamini. Lakini malaika akamhakikishia kuwa yeye ni
shujaa ila ile madhabahu ya Baali aliyokuwa nayo baba yake ndiyo iliyokuwa
inamshikilia hata asijitambue kuwa ni shujaa. Hii inatufundisha kuwa kuna
madhabahu mahali ambayo inakuzuia wewe usifanikiwe kama Mungu alivyokusudia
kwako.
Kwenye madhabahu ile ya nyumbani kwao GIDION kulikuwapo na
ashera pia, ashera ni mti uliopandwa kwa ajili ya kusimamia kitu fulani , Ndiyo
iliyomtesa Gidion kwa mfano mti unaweza
kupandwa kwa jina la mtu na ule mti ukistawi ndipo mtu Yule anapata matatizo
mfano ugonjwa ndiyo maana kuna mtu anakuwa mgonjwa wakati wa masika hii ni kwa
sababu ya ule mti unakuwa umenawili kwa mvua. Kuna mtu yuko mahali hapa na watu
wasiompenda wamempandia mti eidha wa balaa, magonjwa, umasikini, kukataliwa,
kuachwa na kadhalika, lakini leo tunatuma radi na kulipua maashera yote kwa
jina la Yesu.
Kwa hiyo Gidion akaambiwa na bwana wewe ni shujaa unatakiwa
kwenda kupigana vita ila kwanza bomoa madhabahu iliyo kwenye mji huu inayofanya
watu kuwa waoga. Na sisi leo watu wa Hema ya Kinabii Tunaharibu kila ilipo
madhabahu inayolishikilia mokoa, Taifa letu na tunaibomoa kwa jina la Yesu. Leo
lazima watu wote waliolazwa kwenye madhabahu ya nchi hii watatoka na kuelekea
katika hatima zao na mafanikio yao kwa jina la Yesu. Gidion baada ya kuibomoa madhabahu ya
Baali watu wa mji walimtafuta ili wamwuue
lakini baba yake Gidion (YOASHI-BABA WA GIDION) akasema mwacheni baali ajitetee
mwenyewe kwa kubomolewa madhabahu yake, kwa hiyo nakutangazia hata wewe leo
hakuna dhara hata moja litakalokupata kwa kuzibomoa madhabahu za wachawi .
2. Watu waliyowahi kujenga Madhabahu
Mwanzo 8:20, NUHU alipotoka kwenye safina akamjengea Mungu madhabahu,
Hii inaonyesha kuwa kila madhabahu lazima iwe na tukio inaloliwakilisha, kwa
mfano kuna madhabahu za utawala, kwa hiyo huwezi kumwondoa mtawala aliye na
madhabahu imara mpaka uibomoe ile madhabahu ndipo uguse utawala wake. Mwanzo 12:7, Ibrahim alipoongea na bwana
kwamba nchi ile amepewa ndipo alipojenga madhabahu mahali pale ili isimamie
umiliki wake aliopewa kwenye ile nchi,
ndiyo maana hata sasa hakuna mtu anayeweza kuwanyang’anya wa Israel nchi yao
ingawa mataifa mengi wamejaribu kuwaondoa lakini wameshindwa. Mwanzo 12:8,
13:14, Utaona watu kwenye biblia walikuwa wakijenga madhabahu mahali ili isimamie jambo fulani.
Madhabahu ni mahali ambapo wachawi na waganga wa kienyeji
wanakusanyikia , wanapokuwa mahali pale wanatoa Sadaka au kafara za damu na
wanakuja na mashitaka ya kuwashitaki watu na wananza kujadili. Zab 106;37
Hiyo mchawi mmoja
anapeleka shitaka la kumshitaki mtu kwa mfano atasema simpendi fulani kwa
sababu nitajiri sana eti anahela ,au ana watoto wasomi au anapendwa sana na
watu hivyo nataka tumkomeshe kabisa. Kwa
hiyo wachawi wanasema sawa tutamkomesha na ndipo wanapoanza kumtumia mtu
mashetani ya kumharibia maisha yake.
Leo natangaza kuwa madhabahu zote zilizotesa maisha yako
lazima zibomolewe kwa jina la Yesu.
NINAYO NDOTO NA NDOTO YANGU Hab 2:1-3 ni kuwa Falme za dunia zimekuwa
Falme za mwanakondoo na hii imeishakuwa kwa maana madhabahu za kichawi
zilizozuia injili ya Yesu zitabomolewa zote kwa jina la Yesu.
Mchawi anapenda kumshambulia na kumwuua mtu wa karibu yake
kwa mfano kaka, dada, mama, baba nakadhalika. Kwa mfano mtu anataka dada fulani
asiolewe kabisa, anapeleka jina lake kwenye madhabahu na kumwaga kafara, kwa
hiyo kuanzia pale yule Dada hawezi kuolewa kabisa kwa maana madhabahu inakuwa
inaongea fulani asiolewe, asiolewe. Mwingine anaweza kuwekwa kwenye MADHABAHU
YA UOGA, Kwa hiyo hawezi kufanya lolote Kwa kuogopa eidha hasara Kama ni
biashara, ajali kama ni safari, kuachwa kama ni ndoa nakadhalika. Math: 10:36,
Kumwonea wivu mtu Kwa sababu ya mafanikio yake ya kimwili au kiroho – Mwaz
37:3-11
3. Kumchukia mtu bila sababu – Mwaz 37:4
Madhabahu inaweza kuwa kakiwanja Fulani ambapo wachawi
wanakutanikia na kutoa kafara za damu kwa miungu wao. Mtu anaposhitakiwa na
jina lake kutajwa mahali pale ndipo mashetani yanaanza kumwandama na kumharibia
mambo yake, kwa hiyo mtu yule hawezi kufanikiwa hata afanyeje mpaka
atakapoibomoa ile madhabahu. Madhabahu zinapobomolewa watu wanaachiliwa kwa
hiyo wachawi na waganga wa kienyeji wanapata hasara, ndiyo maana Gidion
alitafutwa auawe kwa kuibomoa madhabahu ya baali iliyokuwa nyumbani kwa baba
yake Yoashi. Leo tutabomoa madhabahu iliyokutesa na kuwalaza kwenye hiyo
madhabahu wale waliokuwa wamekulaza kwa jina la Yesu.
MADHABAHU /KIWANJA CHA WACHAWI HUWEZI KUKIONA KWA MACHO
lakini kipo na wachawi wanakutana pale kila usiku na kuwashitaki watu. Ndiyo
maana utaona watu wengi wana matatizo yasiyoisha, Kwa mfano kuna mtu amelazwa
kwenye madhabahu ya kuachwa kwenye ndoa k Kumwonea wivu mtu kwa sababu ya
mafanikio yake ya kimwili au kiroho – MWANZO 37:9-11;
3. Kumchukia mtu na
kuacha kusema naye kwa amani – MWANZO 37:4; wa hiyo utamwona mama ameshaolewa
na wanaume watatu nakuachwa na wote bila sababu ya msingi.
Mungu anapotaka kumwinua mtu anaruhusu apitie mambo magumu
sana kila upande na asione msaada. Ndipo sasa mtu anapoona hana msaada
anakumbuka kumlilia Mungu. Kwa mfano Israel walipokuwa na njaa kali sana mpaka
watu wamefikia hatua ya kula watoto wao,
ndipo Mfalme akasema mwambie nabii Elisha kesho saa saba atakatwa kichwa
asipotabiri kwa habari ya njaa kwenye taifa la Israel. Baada ya kutishwa ndipo
nabii Elisha alitoa unabii kwamba kesho chakula kitapatikana tena kwa bei nafuu
sana kuliko hata kabla ya njaa kutokeaa na kesho yake yakatokea kama vile
Elisha alivyosema. Hii inafundisha kuwa mtu unapopata matatizo usianze kulia
wala kuwalaumu watu bali wakati huo ni wakatiwa kuutafuta uso wa Mungu ili
upate jibu la kukutoa mahali pale.
Usifikiri magumu yanayokupata Mungu amekuacha siyo ni kwamba Mungu
anataka uanze kumlilia na kumtafuta yeye kwa moyo wako wote kwa maana aliona
umeanza kwenda mbali naye.
Kwa hiyo kuna madhabahu ambayo inaweza kuwa imemshikilia mtu
mfano mtu anaweza kuwa amelazwa kwenye madhabahu ya umasikini hata akisoma na
kusafiri nchi zote duniani hawezi kufanikiwa. Kwa hiyo ili mtu huyo afanikiwa
lazima aibomoea ile madhabahu.
Leo kila mtu ataomba
kulingana na udhaifu alio nao kwenye maisha yake kwa mfano mtu mwenye hofu
ataomba akisema kwa jina la Yesu naibomoa madhabahu ya hofu iliyonishikilia na
kuiharibu kafara waliyoitoa kwenye hiyo madhabahu. Kwa jina la Yesu leo naamuka na kuondoka
kwenye madhabhu walioyonilaza kwa jina la Yesu. Na mtu yeyote aliyepeleka jina
langu kwenye madhabahu hiyo namponda kwa jina la Yesu.
Wakati mwingine madhabahu inaweza kuwa siyo kiwanja bali
inakuwa kwenye kitu chochote kile, kwa mfano dada mmoja alikuwa anafanya kazi
kwenye kampuni ya tajiri, siku moja yule dada akaingia kwenye ofisi ya boss
wake na kuona chupa ndogo lakini ndani ya ile chupa yumo yule dada akiwa hai.
Hii inatufundisha kuwa yule dada alikuwa amelazwa kwenye madhabahu ya yule
tajiri , kwa hiyo mafanikio aliyonayo yule tajiri ni kupitia nyota ya yule
dada.
3.0 MAMLAKA TULIYOPEWA NA BWANA WETU YESU KRISTO
Mathayo 10:1, kwa hiyo watu wa Mungu tumepewa mamlaka ya
kutamka na ikawa na leo tunaenda kuzibomoa madhabahu zote kwa jina la Yesu.
Mambo hapa dunia hayatokei yenyewe ila kuna kitu kinafanywa ili yatokee. Na nguvu ya kufanya
mambo yatokee ni uwezo wa mtu wa Rohoni
alionao ndiyo unaleta matokeo mazuri ya mwilini. Kwenye ulimwengu wa
Roho unapotamka kwamba navunja madhabahu iliyonishikilia mahali popote itakuwa
kama utakanyotamka.
4.0 HITIMISHO
4.1 MAOMBI OMBA KWA KUSIMAMIA NENO LA MUNGU,
katika jina la yesu imeandikwa
katika kitabu cha, Yeremia 1:10,Hosea 4:6, Zaburi 18: 1-50, Waamuzi 6:1-40,
Kwa damu ya mwanakondoo naibomoa madhabahu ya wachawi kwa
jina la Yesu, mahali popote walipotaja jina langu napaharibu kwa jina la Yesu,
Naibomoa hali ya kuwa kichaa, naibomoa
madhabahu ya wendawazimu,naibomoa madhabahu ya mikosi kwa jina la Yesu. Mtu
yeyote aliyenilaza kwenye madhabahu yake ya utawala leo naondoka na nakataa
kubaki pale kwa jina la Yesu na nyota yangu naimuru ianze kung’aa.
Nakataa watoto wangu , kazi yangu, ukoo wangu kuwekwa kwenye
madhabahu ya wachawi kwa jina la Yesu. Naibomoa madhabahu ya kifo,
umasikini,uoga na mikosi kwa jina la Yesu. Imeandikwa Gidion aliwapeleka
watumishi wake kumi wakaibomoa madhabahu ya baali, na sisi watumishi wa Mungu
leo tunazibomoa madhabahu zote zilizoshikilia taifa letu na watu kwa jina la Yesu. Imeandikwa bomoeni bomoeni hadi msingini, leo
nabomoa madhabahu zote, madhabahu ya dhiki, magonjwa, umasikini kwa jina la
Yesu. Nabomoa madhabahu ya shaba, udongo, chuma ,mti kwa jina la Yesu. Nakataa
kushikiliwa kwa jina la Yesu, mtu yeyote anayenicontrol kupitia madhabahu
yoyote leo nakaataa kwa jina la Yesu.
Madhabahu ya mabaya iliyoimarishwa naivunja kwa jina la
Yesu, mabaya hayatanipata mimi. Naamuru mizimu, majini, majoka anza kuondoka
kwa maana madhabahu zenu zimebomolewa kwa jina la Yesu. Imeandikwa bwana amenifunga mshipi wa
vita, leo nafanya vita na kuziteketeza
madhabahu zote na nawachinja makuhani wote wa hizo madhabahu.
Naivunja madhabahu inayoninyima promosheni, inayonizuia
nisisafari, inayonizuia nizipate pesa kwa jina la Yesu,. Na kuhani yeyote aliyenipeleka kwenye hizo
madhabahu leo namchinja. Imeandikwa bomoeni bomoeni hadi msingi leo naenda
kubomoa madhabahu za njia panda, porini, bahari . Nainyamazisha damu
iliyomwagwa kwenye madhabahu za wachawi kwa damu ya Yesu.
Ninaamuru kuanzia sasa kila madhabahu inayonena
nainyamazisha kwa jina la Yesu. Kila madhabahu iliyojengwa kwenye nchi ya
Tanzania ili kukamata akili na nia za watanzania leo nakupasua vipanda vipande
kwa jina la Yesu. Naamru na roho zote zilizolazwa kwenye madhabahu zianzae
kuamka kwa jina la Yesu. Nakata kamba zote zinazounganisha watu na madhabahu za
wachawi kwa jina la Yesu.
Nakata ashera zote zilizopandwa kwa majina ya watu kwa jina
la Yesu. Nazilaani ashera zote na kuanzia sasa zianze kukauka kwa jinala Yesu.
Nawateka nyara wasimamizi na makuhani wa madhabahu nawachinja kwa jina la Yesu. Ewe Mungu wa
madhabahu nakukamata na kukuteketeza kabisa na enzi yako yote kwa jina la Yesu.
Leo naamuru mioyo, nafsi, akili na vyote vilivyoshikiliwa kuachiliwa kwa jina
la Yesu. Nauzima moto uliwashwa kwenye madhabahu ya wachawi ili watu wapate
magonjwa, kichaa, umasikini , balaa na mikosi kwa jina la Yesu. Naibomoa
madhabahu iliyojengwa kwenye kichwa, tumbo, kifua kwa jina la Yesu. Naibomoa madhabahu iliyohai
na inayotembea kwa jina la Yesu.
Ufunuo 6:9, kuna roho za watu zinaweza kuwa zimewekwa chini
ya madhabahu. Hata wewe leo unaweza kuwa
hapa lakini roho yako imelazwa kwenye madhabahu, sema leo naivunja madhabahu
iliyonilaza na toka kwa jina la Yesu. Wachawi wa familia wanaweza kumwuuza mtu
na kumpeleka alazwe kwenye madhabahu.
Leo naiteketeza hati ya makubaliano yao ambayo imewekwa kwa jina la
Yesu, hati iliyonifanya niuzwe na nibaki madhabahuni leo naichana na
kuiteketeza kabisa kwa kwa jina la Yesu.
Unaweza kusaidiwa kuharibu madhabahu za kwenu zinazo yatesa
maisha yako wasiliana na Mtu wa Mungu Nabii Samson,
Simu 0756 809 209 Geita,
Samsonmboya18@yahoo.com