SOMO: SIRI YA USHINDI
Na Mtu wa
Mungu Nabii Sam
Maisha
ya mwanadamu yote muongozo Upo Mungu
alishatuwekea unapatikana katika Neno La Mungu hivyo yote tunayoyataka na
kuyatarajia Inatupasa tuyatafute katika Neno la Mungu ,msingi wa somo letu umejengwa katika neno kitabu
cha yohana SURA YA 15 YOHANA 15:9-17. kichwa cha somo letu la leo, ni “siri ya ushindi“, hata hivyo yapo
mengi ya kujifunza ila Roho mtakatifu
ametaka tufahamu katika maeneo haya, Sasa
kama utaanza kusoma katika bibilia yako………
(1)
KAMA VILE BABA ALIVYONIPENDA MIMI (MST. 9)
Maneno
haya, “Kama vile Baba alivyonipenda mimi“, ni maneno aliyoyasema Yesu, muda
mfupi tu kabla ya kusalitiwa na Yuda, na hatimaye kupigwa mijeledi, kutemewa
mate, n.k., na baadaye kusulibishwa.
Yesu
aliyasema haya huku akijua saa yake imefika ya kutendwa haya. Katika hali ya kukabiliwa na mateso makali,
kukanwa na Petro, na kuachwa na wanafunzi wake wote, na hatimaye kufa, bado
alikiri, “kupendwa na Baba“. Kukiri
upendo wa Mungu wakati wote, katika mazingira yoyote yale, ndiyo ilikuwa siri ya ushindi mkubwa wa Yesu
duniani. Wengi wetu hatuko kama
Yesu. Tunapokabiliwa na magumu, dhiki,
mateso, kuachwa na ndugu au wapenzi wetu n.k.; katika mazingira hayo, huwa
hatuukiri upendo wa Mungu kwetu. Huwa
tunaona Mungu hatupendi, hatujali wala hashughuliki nasi. Huwa tunawaza, “Kama kweli Mungu ananipenda,
mbona haya yamenipata?“.
Haitupasi
kuwa hivi. Watu waliotumiwa sana na
Mungu, walikuwa watu wale alioukiri Upendo wa Mungu kwao, katika kukabiliwa na
magumu ya kila aina. Hiki ndicho hasa
kipimo cha kumpenda Mungu. “Akupendaye wakati wa dhiki, ndiye rafiki“,
ni usemi maarufu wa Kiswahili. Mtume
Paulo, yeye naye alikuwa mtu aliyeukiri upendo wa Mungu kwake, katika mazingira
yoyote magumu (WARUMI 8:35-39). Paulo
Mtume alihesabiwa kama takataka za dunia na kupata mateso mengi,
lakini
hata wakati mmoja, hakuwa na mashaka juu ya wito wake au kupendwa kwake na
Mungu, na anatufundisha kujipatia sifa njema katika hali zozote ngumu (1
WAKORINTHO 4:11-13; 2 WAKORINTHO 11:23-28; 1 WAKORINTHO 1:1; 2 WAKORINTHO 1:1;
WAEFESO 1:1; 2 WAKORINTHO 6:4-5). Bwana
atupe neema kumfuata Mtume Paulo kama alivyomfuata Yesu Kristo, ili tupate
mafanikio makubwa. Kama kunasehemu inayomwinua mtu haraka ni wakati anapopitia
mitihani, maana katika hilo kuna kuzawadiwa cheti caha ushindi,
(2)
UPENDO WA YESU KWETU (MST. 9,13)
Yesu
Kristo, anatuhakikishia upendo wake kwetu, tena na tena. Hatuna budi kukaa katika pendo lake tukitafakari
upendo wake mwingi kwetu wakati wote. Ni
upendo mkuu, kwa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Hata hivyo, ni rahisi kwa mtu kufa kwa ajili
ya mtu mwema, lakini ni vigumu kwa mtu yeyote kufa kwa ajili ya mtu mwovu. Yesu alikuwa na upendo wa kipekee sana, pale
alipokufa kwa ajili yetu wenye dhambi, waovu (WARUMI 5:7-8). Bwana atupe neema ya kukaa katika pendo lake
kwa gharama yoyote. Kupuuza pendo hili
ni kukosa shukran
(3)
JINSI YA KUKAA KATIKA PENDO LA YESU (MST. 10)
Pamoja
na Yesu kutupenda upeo, hata hivyo, anatuonya kwamba pendo lake litadumu kwetu
pale tutakapozishika amri zake. Yeye
mwenyewe anatufundisha siri ya Yeye kukaa katika pendo la Baba yake wakti
wote. Alihakikisha anazishika amri zake
wakati wote (YOHANA 8:29). Watu wengi
wanakosa pendo linalodumu kwao kwa sababu ya kuchagua amri za kushika na kuona
kwamba nyingine zimepitwa na wakati.
Visingizio vya kuwa huru na kutokufungwa na sheria, vinavyowafanya watu
wengi kuacha kuzishika amri za Yesu Kristo, na kukosa pendo la Yesu linalodumu
kwao. Bwana ampe neema kila mmoja wetu
kuzishika amri za Yesu Kristo kwa gharama yoyote.
(4) MAKUSUDI YA MAFUNDISHO YA YESU (MST. 11)
Maneno
yote aliyotuambia Yesu, yana lengo la kutupa furaha iliyotimizwa hapa duniani,
na zaidi sana milele na milele. Kwa
kutokuelewa, watu wengine wanafikiri kwamba amri za yesu, zina lengo la
kutufanya wenye huzuni na kuwa mbali na kila namna ya furaha. Furaha iliyotimizwa, inapatikana katika
kuzingatia maneno ya Yesu, na siyo vinginevyo.
Furaha nyingine zote ni za muda tu na siyo furaha halisi.
(5) MPENDANE KAMA NILIVYOPENDA NINYI (MST. 12,17)
Mafundisho
ya Yesu katika siku zake za mwishomwisho katika huduma yake, alikazia sana
kupendana sisi kwa sisi. Muda mfupi
uliopita tulijifunza katika YOHANA 13:34, jambo hilihili. Neno lolote ambalo Yesu analitilia uzito
namna hii na kulisisitiza hivi ni neno la msingi sana katika imani yetu ya
Ukristo. Hatuna budi kupendana kwa
gharama yoyote. Hatupaswi kuchoka
kuchukuliana mizigo katika Makanisa ya Nyumbani, Seksheni na Zoni, na kuona
michango imezidi kwa waliofiwa, na kuipuuza.
Bwana atupe neema hata ya kuutoa uhai wetu (siyo michango tu), kwa ajili
ya ndugu katika Kristo (1 YOHANA 3:16).
(6)
NINYI MMEKUWA
RAFIKI ZANGU (MST. 14-15)
Daudi
na Sulemani, kila mmoja wao alikuwa na mtu MMOJA TU, aliyemwita RAFIKI, katika
wengi waliokuwa karibu nao katika majumba yao ya kifalme (1 SAMWELI 15:37, 1
WAFALME 4:5). Yesu, ni zaidi ya Daudi na
Sulemani, upendo wake kwetu ni zaidi ya nabii yeyote (MATHAYO 12:42). Yesu anawaita watu wote wanaoyatenda
anayowaamuru, RAFIKI zake. Sisi ni
RAFIKI ZAKE! Mtu yeyote hutumiwa uwezo
wake wote kumfurahisha rafiki yake na kumpa mahitaji aliyo nayo. Rafiki zetu wengine, wana mipaka! Rafiki yetu Yesu, anavyote. Furaha yake ni kutupa mahitaji yetu! Hatuna budi kuamini! Kuna jambo jingine la kujifunza hapa. Ingawa Yesu alisema hawaiti tena wanafunzi
wake watumwa, bali rafiki, akawapandisha juu, hata hivyo wanafunzi hao
waliendelea kujiita watumwa (2 PETRO 1:1; YAKOBO 1:1). Hata Yesu akitupandisha juu na kututumia kwa
namna tofauti sana, hatuna budi kuchukua nafasi za chini kana kwamba
hatujapandishwa popote. Bwana atupe
neema kuwa hivi wakati wote.
(7)
YOTE
NILIYOYASIKIA KWA BABA NIMEWAARIFU (MST. 15)
Yesu
Kristo, anatoa kielelezo kwa Mhubiri au Mwalimu wa Neno la Mungu. Yesu Kristo, kama Mhubiri na Mwalimu wa Neno
la Mungu, alifundisha yote aliyoyasikia kwa Baba. Kwa msingi huo huo, ni wajibu wa kila Mhubiri
na Mwalimu wa Neno la Mungu, kufundisha yote aliyotuamuru Yesu, bila kusaza
kitu (MATHAYO 28:19-20). Hatupaswi kutafuta kupendwa na Viongozi wa dini au
watu wa namna yoyote, kwa kuacha kuwaarifu watu KUSUDI LOTE LA MUNGU. Tukitaka kuzitenda kazi alizozifanya Yesu na
kumwona Roho Mtakatifu akitenda kazi pamoja nasi katika huduma zetu, hatuna
budi kumshawishi Mungu kwa kuzingatia jambo hili, bila kujali watu kuondoka
katika makanisa yetu. Mtume Paulo
alizingatia jambo hili hata kama wengi
walimwepuka kutokana na kweli yote aliyofundisha. Hii ndiyo siri ya kutumiwa sana na Mungu
(MATENDO 20:18-20, 26-27; 2 TIMOTHEO 1:15; WAGALATIA 1:10; 4:16-17).
(8) NI MIMI NILIYEWACHAGUA NINYI (MST. 16)
Mtu
hajichagui mwenyewe na kujifanya Mtume, Nabii, Mwinjilisiti, Mchungaji au
Mwalimu. Tukijichagua wenyewe, hatuwezi
kuona amtokeo yanayokusudiwa. Hatuna
budi kuchaguliwa (WAEFESO 4:11). Mtu
akichaguliwa na Mungu katika huduma yoyote kati ya hizi, Mungu atakuwa pamoja
naye kutenda kazi. Tukiwa tumechaguliwa,
hatupaswi kuogopa maneno ya wanadumu kinyume chtu. Tumwogope Mungu tu (MATHAYO 10:27-28). Tukipata kibali kwa Mungu, Mungu huyohuyo
hatimaye atatupa kibali kwa wanadamu kama Mtume Paulo.
(9) SABABU YA KUCHAGULIWA (MST. 16)
Sababu
ya kuchaguliwa katika utumishi wa Mungu ni ili tuzae matunda na matunda hayo
yapate kukaa. Hatuna budi kuipima kazi
yetu ya kuhubiri Injili, kutokana na wale wanaookoka wanaoendelea katika wokovu
na siyo wale tu wanaokata shauri!
Hatukuchaguliwa ili kuwafanya watu wakate tu shauri bali kuwa fanya
wadumu katika wokovu!
(10) UFUNGUO WA KUJIBIWA MAOMBI YOTE (MST. 16)
Pamoja
na vifaa vya kisasa tulivyo navyo leo, Televisheni, Radio, Eropleni, Simu,
Mitambo ya Kupiga Chapa, Vipaza Sauti, Setlaiti n.k.; Wahubiri wengi wa injili duniani hawana uwezo
wa mungu ndani yao kama wale wa Kanisa la Kwanza. Maombi yao hayana nguvu! Ni kwa nini?
Ufunguo wa kujijiwa maombi, ni kuhakikisha matunda ya Injili yanakaa! Tukiwaambia watu waokoke na kubaki katika
madhehebu yao yaliyojaa sanamu, tunakuwa tunaukosa ufunguo huu. Matunda haya yatadumu namna gani katika
kusanyiko lililojaa giza? Tugeuke na
kuuchukua ufunguo huu ili dunia hii ipinduliwe kizazi hiki. kiovu
**********************************************************************************
Wasliana
na Mtumishi wa Mungu kwa ushaushauri na maombezi