SOMO: TAA YA MWILI :( J2:1)
SOMO : TAA YA MWILI
Utangulizi Tutajifunza maana ya Taa,na Mwili,kazi na faida ya taa ya mwili
Luka 11:34 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako
likiwa safi, mwili wako wote unao mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao
una giza.
1Wakoritho 2:14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.
1Wakoritho 2:14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.
Zaburi 119:18 -22 Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu
yatokayo katika sheria yako.
Yohana 8:12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi
ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa
na nuru ya uzima.
2wakoritho 3:18
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana,
kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu
hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
2Wakoritho 4:6 Kwa
kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni
mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.
Waefeso 1:18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue
tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake
katika watakatifu jinsi ulivyo;
SOMO: KUWA HODARI (J2:2)
Utangulizi Tutajifunza maana ya kuwa
Hodari,Sababu na faida ya kuwa Hodari
Yoshua 1:7 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie
kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa
Zaburi 27:1 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope
nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
Isaya 40:29
Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
Zaburi 73:26 Mwili
wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu
yangu milele.
Warumi 8:31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo
upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Zaburi 44:5,Warumi 8:37, Lakini katika mambo hayo yote
tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. 1Nyakati 22:16,Zaburi 118:6
Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
SOMO: WATU WALIOBARIKIWA (J2:3)
Utangulizi Tutawafahamu watu waliobarikiwa na Sababu ya wao kubarikiwa na sisi JE?
Mathayo 25:34 Kisha
Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba
yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
Luka 12:31 Bali
utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa. Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba
yenu ameona vema kuwapa ule ufalme
Yakobo2:5 Ndugu
zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe
matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?
Warumi 8:17 na
kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo;
naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa
sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.
Yohana 16:27 kwa
maana Baba mwenyewe awapenda kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, na kusadiki ya
kwamba mimi nalitoka kwa Baba.
Waibrani 11:16 Kwa
imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita
wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. Yeye ashindaye
atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na
wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu
yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
SOMO: FURAHA KATIKA ROHO MTAKATIFU (J2:4)
Utangulizi Tutaijuwa furaha ya kweli ndani ya Roho Mtakatifu,
Wagalatia 5:22
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema,
fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Warumi 14:17 Maana
ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika
Roho Mtakatifu. Kwa kuwa yeye
amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na
wanadamu.
1Petro 1;18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu
viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa
mlioupokea kwa baba zenu;
2Wakoritho 6:9 kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana;
kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa; kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye
furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu
wenye vitu vyote.Warumi 5:3 Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki
pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; Waibrania
12;2,Yohana 15:11,2Wakoritho 1:5,waphilip 4:4,Nehemia 8;10,Zaburi 16:11,Ufunuo 7:17
SOMO:KUMWESHIMU MUNGU KWA MALI
ZAKO(J2:5)
Utangulizi: Tutajifunza namna ya kumweshimu Mungu pamoja na
mali zetu
Mithali 3;9 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya
mazao yako yote. Ndipo ghala zako
zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya
.2Wakoritho
9:6 6 Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio
na uwezo wa kutokufanya kazi? Ni askari
gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye
mizabibu asiyekula katika matunda yake?
1Wakoritho16:2 Siku ya
kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa
kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
Waibrania 6:10 Maana
Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa
jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali
mkiwahudumia.Warumi 12:1,2Wakoritho 5;14-15,1Wakoritho
10:21 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu
wa Mungu
SOMO HATARI YA WINGI WA MANENO (J2:6)
Utangulizi
Mithali 10:19 Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu;
Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili. Ulimi wa mwenye haki ni kama fedha teule;
Moyo wa mtu mbaya haufai kitu.
Yakobo 1:19 Hayo
mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si
mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Mithali 16:32 Asiye
mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko
mtu atekaye mji
Yakobo 3:2 Maana
twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo
ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.Mathayo 12:37,Zaburi 141:3,1Petro
2:21-23,Waibrania 12:3,
Ufunuo 14:5 5 Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.