Powered By Blogger

Thursday, 12 February 2015

Namna ya kuishinda dhambi


USHINDI JUU YA DHAMBI,


 

 

 Kuishinda dhambi hakuna mtu chini ya jua anayeweza kuishinda Dhambi kwa ujanja wake au kwa nguvu zake pasipo kusaidiwa na Mungu,  siku zote anayetuwezesha kuishinda Dhambi ni Mungu peke yake,

 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana Wewe upo pamoja nami.

 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. —Wafilipi 4:13, 19

 Namna ya kuishinda Dhambi,

 1 Wakorintho 10:13

 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

 Waebrania 4:16

 Basi na tukikaribie kiti cha flee-ma kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

  2 Timotheo 2:22

 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

 1 Yohana 1:7

 Bali tukienenda nuruni, kama yeye ahivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

 Warumi 6:11

 Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

 

 Yakobo 4:7

 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

 Zaburi 119:11

 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi.

 Nguvu ya maombi

 Zaburi 27:8

 Uliposema, Nitafuteni uso Wangu, Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta.

 Zaburi 62:8

 Enyi watu, mtumainini sikuzote, ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.

 Yeremia 17:14

 Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.

  1 Wathesalonike 5:17, 18

 Ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika KristoYesu.

 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. —Yakobo 1:5

  Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. —Yohana 15:7

  Zaburi 34:4

 Nalimtafuta BWANA akanijibu, akaniponya na hofu zangu zote.

 Zaburi 66:18; 25:11

 Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia. Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.

Jiweke tayari kwa ujio wa kristo Yesu

 
 1 Wathesalonike 4:16, 17

 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.

 
 2 Wakorintho 7:1

 Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.

 
 1 Yohana 2:28

 Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake katika kuja kwake.

 

 Yakobo 5:8, 9Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. Ndugu, msinung’unikiane msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.

 Luka 12:40

 Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.

Kujazwa na Roho wa Mungu ni jambo la muhimu pia katika maisha ya mwanadamu,

 
 Mithali 1:23

 Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; tazama, nitawamwagia roho yangu, na kuwajulisheni maneno yangu.

 
Matendo 2:38

 Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

 
Waefeso 5:18-21

 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.

 

 Wafilipi 2:13

 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.

1 Wakorintho 3:16; 6:2
Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. na yeye atakaye liharibu Hekalu langu nami nitamuharibu, ukivuta sigara,ukifanya ukahaba,ukinywa pombe,ukilinajisi hekalu la Mungu yaani mwili wako naye Bwana atauharibu, Hebu fahamu hivi alichokiharamisha Mungu mwanadamu Hawezi kukihalalisha au kukitakasa kwa namna yeyote ile,

 
Na kunzuri zaidi Mungu Hakuwahi kubadilika wala siyo kigeu geu alilolikataza miaka elfu tatu mpaka sasa hajaliruhusu  na aliloliruhusu pia mwanadamu hawezi kulizuwia, kuzuwia kwa mwanadamu ni kujiangamiza, kama ilivyo kuhalalisha asichoalalisha ukaangamia ndivyo na kuzuwia alicho alalisha ishi kama anavyoagiza si kama unavyo taka wewe kuishi,kwasababu hayupo ajuwaye baada ya Dakika tano nini kitamtokea,

 hakuna mtu aliyejichaguwa awe alivyo hivi sasa hata kuzaliwa kila mmoja alijikuta yuko kama alivyo awe ni mwanaume,au mwanamke hivyo hayupo anayeweza kutamba kwa mwingine wala kwa chochote alicho nacho, kama ni kutamba Bwana anaruhusu mtu atambe kwaajili ya kumfahamu yeye,, Je unahitaji ushauri au maombezi fika hema ya kinabii nyankumbu au piga simu 0756 809 209

Ninawezaje Pata amani?

Unawezaje kupata amani? Baba Nabii akifunua siri ya kuwa na amani kama ya kwake aliyonayo Utangulizi kazi kubwa kabisa kwa Mwanadamu...