USHINDI JUU YA DHAMBI,
Kuishinda dhambi hakuna mtu chini ya jua
anayeweza kuishinda Dhambi kwa ujanja wake au kwa nguvu zake pasipo kusaidiwa
na Mungu, siku zote anayetuwezesha
kuishinda Dhambi ni Mungu peke yake,
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde
katika njia zako zote. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
sitaogopa mabaya; kwa maana Wewe upo pamoja nami.
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye
nguvu. Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri
wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. —Wafilipi 4:13, 19
Namna ya kuishinda Dhambi,
1 Wakorintho 10:13
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo
kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita
mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze
kustahimili.
Waebrania 4:16
Basi na tukikaribie kiti cha flee-ma kwa
ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
2 Timotheo 2:22
Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate
haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo
safi.
1 Yohana 1:7
Bali tukienenda nuruni, kama yeye ahivyo
katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha
dhambi yote.
Warumi 6:11
Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu
kwa dhambi, na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.
Yakobo 4:7
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye
atawakimbia.
Zaburi 119:11
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije
nikakutenda dhambi.
Nguvu ya maombi
Zaburi 27:8
Uliposema, Nitafuteni uso Wangu, Moyo wangu
umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta.
Zaburi 62:8
Enyi watu, mtumainini sikuzote, ifunueni mioyo
yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.
Yeremia 17:14
Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe,
nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.
1 Wathesalonike 5:17, 18
Ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo;
maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika KristoYesu.
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na
aombe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
—Yakobo 1:5
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu
yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. —Yohana 15:7
Zaburi 34:4
Nalimtafuta BWANA akanijibu, akaniponya na
hofu zangu zote.
Zaburi 66:18; 25:11
Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana
asingesikia. Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, maana ni
mwingi.
Jiweke tayari kwa ujio wa kristo Yesu
1 Wathesalonike 4:16, 17
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka
mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu;
nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai,
tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani;
na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
2 Wakorintho 7:1
Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo,
na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza
utakatifu katika kumcha Mungu.
1 Yohana 2:28
Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili
kusudi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake katika
kuja kwake.
Yakobo 5:8, 9
Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana
kuja kwake Bwana kunakaribia. Ndugu, msinung’unikiane msije mkahukumiwa.
Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.
Luka 12:40
Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani
ndipo ajapo Mwana wa Adamu.
Kujazwa na Roho wa Mungu ni jambo
la muhimu pia katika maisha ya mwanadamu,
Mithali 1:23
Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; tazama,
nitawamwagia roho yangu, na kuwajulisheni maneno yangu.
Matendo 2:38
Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake
Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho
Mtakatifu.
Waefeso 5:18-21
Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi;
bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku
mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote
kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; hali mnanyenyekeana
katika kicho cha Kristo.
Wafilipi 2:13
Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani
yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
1 Wakorintho 3:16; 6:2
Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu,
na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa
basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. na yeye atakaye liharibu Hekalu langu
nami nitamuharibu, ukivuta sigara,ukifanya ukahaba,ukinywa pombe,ukilinajisi
hekalu la Mungu yaani mwili wako naye Bwana atauharibu, Hebu fahamu hivi
alichokiharamisha Mungu mwanadamu Hawezi kukihalalisha au kukitakasa kwa namna
yeyote ile,
Na kunzuri zaidi Mungu Hakuwahi kubadilika
wala siyo kigeu geu alilolikataza miaka elfu tatu mpaka sasa hajaliruhusu na aliloliruhusu pia mwanadamu hawezi
kulizuwia, kuzuwia kwa mwanadamu ni kujiangamiza, kama ilivyo kuhalalisha asichoalalisha
ukaangamia ndivyo na kuzuwia alicho alalisha ishi kama anavyoagiza si kama
unavyo taka wewe kuishi,kwasababu hayupo ajuwaye baada ya Dakika tano nini
kitamtokea,
hakuna mtu aliyejichaguwa awe alivyo hivi sasa
hata kuzaliwa kila mmoja alijikuta yuko kama alivyo awe ni mwanaume,au mwanamke
hivyo hayupo anayeweza kutamba kwa mwingine wala kwa chochote alicho nacho,
kama ni kutamba Bwana anaruhusu mtu atambe kwaajili ya kumfahamu yeye,,